Google tag

mercredi 24 avril 2013

Rich Mavoko - One Time

new song of

Rich Mavoko - One Time

Hadiyth Ya 6

Hadiyth Ya 6

Mmoja Katika Waja Wangu Ameamini Na Mmoja Amekufuru


عَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ الْجُهَنِيِّ قَالَ صَلَّى لَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلَاةَ الصُّبْحِ بِالْحُدَيْبِيَةِ عَلَى أَثَرِ سَمَاءٍ كَانَتْ مِنْ اللَّيْلِ فَلَمَّا انْصَرَفَ أَقْبَلَ عَلَى النَّاسِ قَالَ:  ((هَلْ تَدْرُونَ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ؟)) قَالُوا اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ قَالَ(( أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ بِي وكَافِرٌ,  فَأَمَّا مَنْ قَالَ مُطِرْنَا بِفَضْلِ اللَّهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَذَلِكَ مُؤْمِنٌ بِي كَافِرٌ بِالْكَوْكَبِ وَأَمَّا مَنْ قَالَ مُطِرْنَا بِنَوْءِ كَذَا وَكَذَا فَذَلِكَ كَافِرٌ بِي مُؤْمِنٌ بِالْكَوْكَبِ)) البخاري والنسائي

Kutoka kwa Zayd bin Khaalid Al-Juhaniyy رضي الله عنه   ambaye amesema: Mtume صلى الله عليه وسلم alituswalisha Swalah ya Alfajiri (huko) Al-Hudaybiyah baada ya kunyesha mvua usiku. ِAlipomaliza aliwaelekea watu akasema: ((Je, mnajua Mola wetu kasema nini?)) Watu wakasema Allaah na Mjumbe Wake ni wajuzi bora. Akasema: ((Mmoja katika waja Wangu ameamka asubuhi akiwa ameniamini na mmoja amenikufuru. Ama aliyesema: tumepewa mvua kwa fadhila za Allaah na Rehma Zake, huyo ameniamini Mimi na amezikana nyota; ama aliyesema: tumepewa mvua kwa nyota kadhaa wa kadhaa huyu amenikufuru Mimi na ameamini nyota)) [Al-Bukhaariy na An-Nasaaiy]