Mshindi ya tuzo la Nobel raia wa Nigeria Wole Soyinka, ametimiza ahadi ya kuirarua green card yake kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
Mwezi uliopta mshindi huyo wa tuzo la fasihi alisema kuwa angeirarua green card, ambayo humpa mtu kibali cha kuishi nchini Marekanai ikiwa Dionald Trump angechaguliwa kuwa rais wa Marekani.
Aliliambia shirika la AFP mjini Johannesburg kuwa kutokana na vile Trump ameshinda, basi ametekeleza alichokisema
"Tayari nishafanya, nimetoka Marekani , nimefanya kile nilisema ningekifanya, nilitupa green card yangu , nimerudi penye ninastahili kuwa," alisema Soyinka.
Hata hivyo Soyinka hawashauri watu wengine kufuata mkondo huo.