Refarii Facundo Tello ameingia kwenye vichwa vya vyombo vya habari Duniani baada ya kutoa kadi nyekundu kumi (10) katika dakika za mwisho wa mchezo wa kombe la Ligi Nchini Argentina 🇦🇷. Aidha, mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya (1-1) hadi dakika ya tisini (90) kisha kuongezwa dakika 30 ambapo Refarii Tello alitoa kadi hizo nyekundu kutokana na matukio yaliyotokea Uwanjani hapo baina ya klabu ya Boca Juniors ambao walipoteza mchezo huo dhidi ya Racing (1-2).
Refarii huyo ni miongoni mwa Waamuzi watakaochezesha kwenye michuano ya Kombe la Dunia huko Qatar na tayari ameshatoa kadi za njano 612 pamoja na nyekundu 45 huku akiwa amechezesha michezo 118 katika maisha yake ya Urefa.