Google tag

mercredi 17 mai 2017

Wafungwa wauawa wakijaribu kutoroka jela DRC

Idadi ya wafungwa wasiojulikana wameuawa kwa kupigwa risasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mapema leo baada ya jaribio la kuhepa kutoka gereza kubwa lililoko mjini Kinshasa.
Waziri wa sheria nchini humo, Alexis Thambwe Mwamba amesema baadhi ya wafungwa wapatao 100 wamekamatwa huku wengine hamsini na watano wakiendelea kusakwa.

Miongoni mwa wanaodaiwa kufanikiwa kutoroka ni mfungwa mmoja aliyekuwa akitumikia kifungo cha maisha gerezani kwa mauaji ya rais wa zamani wa DRC, Laurent Kabila.
Maafisa wa usalama wameanzisha oparesheni kali mjini Kinshasa ili kuwakamata wafungwa hao.
Aidha, baadhi ya wafungwa wameuawa kwa kupigwa risasi wakijaribu kukimbia .
Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema amewaona maafisa wa shirika la Msalaba Mwekundu, wakikusanya miili yao.
Miili ya waliofariki imepelekwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti mjini Kinshasa.

Hii sio mara ya kwanza kwa wafungwa kutoroka kutoka magereza nchini DRC kwani Januari mwaka uliopita, kisa kama hicho kilishuhudiwa mashariki mwa taifa hilo ambapo wafungwa hamsini walitoroka.
Miongoni mwa waliofanikiwa kutoroka ni wafungwa wa kesi za mauaji na ubakaji.
Mamlaka za magereza zimelaumiwa kwa visa hivyo kwa ulegevu huku magereza mengi yakiwa na msongamano.
Mashirika ya kutetea haki za kibanadam yanalaumu idara ya mahakama kwa kutokamilisha kesi haraka.

Sheddy Clever aiomba serikali kutumbua maprodyuza feki

Mtayarishaji wa muziki nchini, Sheddy Clever ameitaka serikali iweke sheria na viwango vya kudhibiti watayarishaji wa muziki feki ambao ni chanzo cha kusababisha nyimbo kutodumu mda mrefu katika tasnia hali inayopelekea kushuka kwa muziki bongo.

Sheddy amedai serikali inapaswa pia kusimama na kuangalia maslahi ya watayarishaji wa muziki kwani wamekuwa wakiwatajirisha wasanii huku wao wakibaki kwenye maisha yale yale.
“Maprodyuza feki ni wengi sana wale waliopo real ni wachache sana. Zamani kina P -Funk walikuwa wanatengeneza nyimbo zinadumu muda mrefu na ni kali lakini za sasa hivi imebidi ma director wa video wawe wabunifu kutengeneza video kali ili wimbo uonekane ni mzuri,” Sheddy alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.

Aongeaza, “Upande wa maslahi inabidi serikali ijipange ituwekee maslahi mazuri kwani mtayarishaji wa muziki kama anahitaji maisha mazuri itambidi awe anakazi nyingine na siyo kutegemea production tuu. Unaweza ukawa na hit kibao redioni lakini maisha yako yakawa ya tabu sana,”
Mtayarishaji huyo ameshatengeneza hit nyingi ikiwemo ‘Marry You’ ya Diamond na Ne-Yo.

Memphis Depay azua gumzo katika tuzo ya mchezaji bora Ufaransa

Mshambuliaji wa klabu ya Lyon, Memphis Depay, amepokea tuzo yake ya bao bora la mwaka. Wakati akienda kupokea tuzo hiyo ya heshima, ameonekana kuvalia Jacket lake mithili ya Msanii nguli wa Pop Duniani, Michael Jackson.

Nyota huyo wa timu ya taifa ya Uholanzi amenyakuwa tuzo hiyo baada ya kufunga bao akiwa umbali wa nusu ya Uwanja.
Depay mwenye umri wa miaka 23 amekuwa na mafanikio toka alipoondoka katika klabu ya Manchester United na kujiunga na klabu ya Lyon ya Ufaransa. Muonekano wake katika tuzo hizo umewaduwaza walio wengi na kuwavutia Ukimbini hapo kwa namna alivyovalia ikiwa ni jambo ambalo halikutarajiwa na wengi.
Nyota wa zamani wa Uholanzi Frank de beor aliwahi kumuonya Depay kwa kumtaka aweke akili yake zaidi uwanjani kabla ya kujiingiza katika mambo mengine ya nje ya uwanja.

Baada ya kufunga mabao 5 katika michezo 15 aliyoingia uwanjani, ni wazi sasa Depay anahisi ni muda wake muafaka way yeye kurudi katika ulimwengu wake wa mitindo anaoonekana kukosa kwa muda mrefu sasa.