Alibaba

vendredi 10 mai 2013

Burundiano



BI KIDUDE KAFA FUKARA

KUSOMA HABARI ZOTE BOFYA HAPA
Stori; Imelda Mtema
MAISHA ya mwisho ya mwanamuziki maarufu wa taarab na fundi wa kufunda unyago nchini, Fatma binti Baraka ‘Bi Kidude’ hakika yalitia simanzi, Ijumaa Wikienda lina ripoti ya kuumiza moyo.
Bi Kidude na Matalii
Bi Kidude, pamoja na kutamba kwa nyimbo zake na kufanya ziara za mara kwa mara sehemu mbalimbali duniani, amekufa akiwa fukara huku watu wachache wakinufaika kwa kipaji chake cha uimbaji.
Dirisha la kwanza kushoto ndio chumba achokuwa akilala...
WAOMBOLEZAJI WAMWAGA MACHOZI
Baadhi ya waombolezaji waliofika nyumbani kwake, Raha Leo mjini Unguja kwa ajili ya kumsitiri, walimwaga machozi pale walipokutana na hali duni ya maisha ya mwanamuziki huyo mkongwe.
Godoro alilokuwa akilalia Bi kidude likiwa limetupwa nje

GODORO CHAKAVU
Mwandishi wa gazeti hili aliyekuwa Zanzibar alipata fursa ya kuyaona mazingira aliyokuwa akiishi mwanamuziki huyo, hakika ilitia uchungu.
Bi Kidude ambaye alifanya ziara nyingi za kimataifa, alikuwa akilalia godoro chakavu lililotoboka na kutawaliwa na uchafu katika kila pembe.
GODORO LATUPWA
Godoro hilo, ilibidi litupwe baada ya kifo chake ili waombolezaji wengine wasilione na kubaini ukweli wa maisha duni ya Bi Kidude ambaye alifariki dunia Aprili 17, mwaka huu akiwa na umri wa miaka 104.
Mbali na godoro, chumba cha Bi Kidude hakikuwa na hadhi yake, kilikuwa kichafu na kulazimika kusafishwa haraka ili kusitiri aibu ya marehemu ambayo ilisababishwa na watu waliokuwa wakimtumia kuchuma fedha kwa mgongo wake.

WATU WALIKUWA WAKIMCHUNGULIA
Jambo la kushangaza ni kwamba hadi anaaga dunia Jumatano iliyopita na kuzikwa kesho yake, nyumba ya Bi Kidude haikuwa imemalizika kujengwa.
Nyumba hiyo ilikuwa imekamilika upande mmoja tu bila ya kujua fedha za shoo na matamasha mbalimbali makubwa alizokuwa akizipata zilikuwa zikienda wapi.
Dirisha la chumba chake wavu ulikuwa umekatika na kufanya mbu wa kumwaga kujazana chumbani mwake huku vibaka na watu wengine wasio na tabia njema kuweza kumchungulia akiwa ndani wakati wa usiku.

ALIKUWA KAMA OMBAOMBA
Enzi za uhai wake, waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali duniani na watalii walipomtembelea Bi Kidude, kitu cha kwanza aliwaomba fedha za kununulia sigara hivyo kuonekana kama ombaomba.
Mbali na fedha za sigara pia angeweza kuomba kiasi kingine cha fedha kwa ajili ya matumizi yake mengine.

TATIZO NI NINI?
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mtoto wa kaka wa marehemu Bi Kidude, Baraka Othuman Baraka alikiri kwamba shangazi yake alikufa akiwa hohehahe.

ELIMU YATAJWA
“Udhaifu wa kwanza ambao watu wengi hasa waandaaji wa matamasha makubwa ndani na nje ya nchi walioutumia kuvuna fedha za Bi kidude ni elimu kwani hakwenda shule zaidi ya Madrasa,” alisema Baraka.
Baraka alisema kuwa watu wengi walipata mwanya huo na kumtumia shangazi yake na kisha kumuacha fukara bila ya kumwachia faida yoyote.
“Wewe umesema nyumba haijamaliziwa, hebu angalia hata upande ulioisha haujapigwa hata plasta,” alisema Baraka kwa majonzi.
Baraka aliongeza kuwa kitu ambacho kinamuumiza ni kuona Bi Kidude amekuwa akifanya matamasha ya ndani na nje lakini maisha yake yaliendelea kuwa duni.
“Watu walimtapeli sana Bi Kidude, kuna waliokuwa wakimfanyisha matamasha kila mwaka, Bi Kidude alikuwa akienda kushinda ofisini kwao ili wampatie fedha za kununulia godoro, nao wakawa wanamuahidi kwamba watampa lakini mpaka anafariki dunia hakuambulia chochote,” alisema Baraka.

MATIBABU DUNI
Baraka ameliambia Ijumaa Wikienda kwamba, ndugu walikuwa wakihangaika na Bi Kidude katika hospitali za kawaida tu pale alipoumwa, wala hawakuwahi kupata msaada mkubwa wa matibabu pamoja na kwamba alikuwa kama nembo ya Zanzibar.
“Wageni wengi waliokuwa wakija Zanzibar walikuwa wakitaka kumuona Bi Kidude, lakini ndiyo hivyo hakuna aliyemjali katika suala la matibabu,” alisema Baraka.
Pamoja na  lawama hizo, Baraka alimshukuru Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein ambaye aliwahi kumtembelea marehemu na kumuachia kiasi cha fedha wakati wa Sikukuu ya Eid El Fitr.

LAWAMA ZA NDUGU?
Watu wengi msibani walitupa lawama kwa ndugu wa marehemu kutokana na kutomwangalia kwa karibu na kuratibu shughuli zake za muziki, Baraka anasemaje?
“Kila ndugu tulipojaribu kutaka kuingilia kati juu ya maslahi ya marehemu tulionekana viherehere, baadhi ya watu walikuwa wakituona kama vile tunawabana na kuanza kutoa shutuma kwetu,” alisema.

FEDHA ZAKE ZAYEYUKA BENKI
Kama vile haitoshi, Baraka alidai kwamba kuna watu walijidai kwamba walikuwa wakimwekea Bi Kidude fedha benki lakini kila walipowauliza ilikuwa ni ugomvi hivyo mbali na nyumba kuukuu aliyokuwa akiishi, hakuna utajiri wowote alioacha hivyo ni changamoto kwa wasanii wa Kibongo.
“Sijui hizo fedha kama zipo kweli na hata zikiwepo zitasaidia nini wakati mtu mwenyewe ameshafariki?” alihoji kwa hasira.

NENO LA IJUMAA WIKIENDA
Watu wengi wanatajwa kuhusika kumhujumu mkongwe huyo kwa kumfanyisha kazi bila malipo, ni rai yetu kuwa wahusika watapeleka kiasi cha fedha walichonacho katika familia yake. 

MAMA KANUMBA: CHONDECHONDE, KABURI LA MWANANGU LISIGEUZWE MTAJI

Kaburi la marehemu Steven Kanumba.

BAADA ya siku za hivi karibuni kubainika kuwa baadhi ya vijana wanaolinda makaburi ya Kinondoni wamegeuza mtaji kaburi la aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, mama mzazi Flora Mtegoa amewaomba wahusika kuacha mchezo huo mara moja.
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Akizungumza kwa huzuni mama Kanumba alisema alihuzunishwa sana na kitendo hicho cha kaburi la mwanaye kugeuzwa mtaji na kumtaka mtu yeyote atakayetozwa pesa aripoti polisi mara moja.
“Inaniuma sana na naiomba serikali na watu wengine wanisaidie jamani kwa sababu wanaofanya biashara hiyo ya kulipisha watu kwa ajili ya kuliona kaburi wanakosea,” alisema Mama Kanumba.
Hivi karibuni ilibainika kuwa baadhi ya vijana wanaotunza makaburi ya Kinondoni wanatoza shilingi 5,000 kwa watu wanaotoka mikoani kwa ajili ya kuliona kaburi la Kanumba na kupiga picha.

Kibanio WAREMBO watatu wanaodaiwa kuwa ni madenti wa chuo kikuu kimoja jijini Dar


WAREMBO watatu wanaodaiwa kuwa ni madenti wa chuo kikuu kimoja jijini Dar, waliojitambulisha kwa jina mojamoja, Rachel, Neema na Suzan, wamekumbana na balaa zito baada ya kupokea kibano cha kutosha, Ijumaa lina mkanda kamili.
Soo: Warembo hao watatu wakificha sura zao kwa aibu baada ya kubambwa na kushushiwa kichapo getini kwa kigogo.
Tukio hilo lililonaswa laivu na gazeti hili lilitokea maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar, usiku wa saa 8:00, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo madenti hao walipokea kibano ‘hevi’ kutoka kwa Polisi Jamii.
Kipondo: Madenti hao baada ya kusurubiwa na Polisi Jamii.
KERO
Warembo hao walifikwa na kasheshe hilo baada ya kugeuka kero kwenye geti la kigogo mmoja (jina linahifadhiwa kwa sababu maalum) kwa kuwa walionywa mara kadhaa kuacha kupanga foleni katika eneo hilo na kujihusisha na vitendo vya ngono.
“Unajua walikuwa kero sana. Yaani asubuhi kukicha utakuta mipira ya kiume imetapakaa kila sehemu. Mbaya zaidi utakuta watoto wakicheza mchana wanaokota hiyo mipira ya kiume na kupuliza kama puto,” alisema shuhuda mmoja aliyeamshwa na makelele ya warembo hao wakati wakila kibano.
Vilio: Warembo hao wakilia baada ya kichapo.
Aliendelea: “Unajua wakikaa hapa ni hatari tupu kwani wanaume wanaokuja kuwafuata wanaweza wakatudhuru kwa sababu hatuwajui.”

MALALAMIKO
Katika tukio hilo, walinzi hao wakiwa kwenye doria, walipokea malalamiko kwa mara 1000, kutoka kwa kigogo huyo akiomba msaada wa kuwaondoa warembo hao getini kwake wanaodaiwa kujiuza eneo hilo.
LENGO KUMNASA KIGOGO
Habari nyingine zilieleza kuwa wadada hao wamekuwa wakiweka mitego yao nje ya nyumba hiyo ikidaiwa kwamba lengo ni kumnasa kigogo huyo ili kumuuzia biashara yao kwa kuwa ni ‘mkataji’ mzuri wa mkwanja.
Mbali na hilo, pia ilidaiwa kuwa wanaume wapenda ngono rejareja na hatarishi huwafuata eneo hilo kupata huduma yao.
Ilidaiwa kuwa walinzi hao walielezwa kuwa katika kukuza biashara hiyo haramu, warembo hao wamekuwa wakiwabugudhi wakazi wa eneo hilo hadi kufikia hatua ya kuwagongea madirishani na kusimamisha magari hovyo.
WAONESHA NYETI
Huku wakijua wamepata wateja, kundi la kinadada hao wakiwa na vinguo vya kimitego na wengine kujifunua na kubaki nusu utupu ili kuwaonesha wanausalama hao nyeti zao wakijua ni wateja ndipo wakakutwa na kasheshe hilo.

KIBANO
Wanausalama hao, bila kuchelewa waliwazingira warembo hao na kuwanasa kisha kuwapa kibano lakini katika purukushani hiyo wengine walifanikiwa kupata upenyo na kuchoropoka.
WAFUNGA MTAA
Katika kibano hicho, makelele ya warembo hao yalisababisha watu kuamka na kufunga mtaa.
Kutokana na timbwili hilo la akina dada hao kuwa zito, iliwabidi polisi hao jamii watumie nguvu ya ziada kuwatuliza kabla ya kuwapeleka mbele ya sheria.
FUNDISHO
Baada ya warembo hao ‘kutaitiwa’ walipakizwa kwenye Bajaj na kupelekwa kituo cha polisi ili wafikishwe mahakamani.
Kwa kashikashi waliyopata ni dhahiri kuwa kilichowapa madenti hao ni fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Mashabiki Morogoro wamlilia Ferguson


Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson.

MASHABIKI wa Manchester United ya England wa mkoani morogoro wamesema ni pigo kubwa kwa timu yao baada ya Kocha Sir Alex Ferguson kutangaza kung’atuka kuifundisha timu hiyo baada ya msimu huu.
Wakizungumza na Championi Ijumaa mjini hapa, baadhi ya mashabiki hao walisema Ferguson alikuwa mtu muhimu na nguzo imara ndani ya Man U, hivyo kuondoka kwake kutaacha pengo kubwa katika klabu hiyo.
Walisema kocha huyo alikuwa mstari wa mbele kuitafutia mafanikio timu hiyo ikiwa ni pamoja na kudumisha nidhamu katika kikosi cha United.
“Kwa kweli tumepata pigo kubwa sana lakini hatuna jinsi, tunapaswa kuheshimu maamuzi yake,” alisema Mangi Chang’waro.
Hata hivyo, mashabiki hao walisema wanaomba apatikane kocha mwingine mzuri atakayeendelea kuipa mafanikio timu hiyo.