Google tag

mercredi 2 novembre 2016

Esma Platnumz Avunja Ukimya, Afunguka Kuhusu Wazazi Halisi wa Diamond Platnumz

Dada wa msanii Diamond platnuz Esma Platnumz amesema hakuwahi kumtabiria wala kutegemea kuwa kaka yake Diamond angekuja kuwa mtu maarufu kimataifa japo alikuwa akionesha kupenda muziki tangu akiwa mdogo.

Hata hivyo Esma amesema maswala yanayoandikwa kwenye magazeti kuhusiana na Baba yake siyo ya kweli kwa kuwa yeye anamfahamu baba yake mzazi na mtu aliyejitokeza kwenye magazeti siyo baba yake na hamfaham kabisa.

Pia Esma hakusita kuongelea taarifa zilizozagaa kwamba mama Daimond hana mahusiano mazuri na wifi yao Zari na kusema hawana tatizo lolote na wifi yao na hakuna mzazi asiye furahia wajukuu  hivyo watu wanayoyaona katika magazeti siyo ya kweli na wasiyatilie mkazo, huku akimalizia kwa kusema kuwa anampenda mume wake Petit Man

Eden Hazard élu joueur du mois en Premier League par les supporters

Eden Hazard a été choisi joueur du mois d'octobre en Premier League par les supporters, a communiqué l'association des footballeurs professionnels (PFA), mercredi.

Eden Hazard était nominé avec Joe Allen, Dele Alli, Charlie Austin, Theo Walcott et Callum Wilson. Ce titre honorifique n'est pas à confondre avec l'officiel prix de la Premier League intitulé aussi "Joueur du mois" qu'Eden Hazard n'a pas encore pu gagner. Eden Hazard avait par contre été élu "Joueur de la Saison 2014-2015" en Premier League.

Kicheko

Umeshawai kukaa gheto mwenyewe alafu ghafla unasikia halufu ya ushuzi wakat ww hujajamba wala nini 
HAPO NDIO UTAKUMBUKA ILE NYIMBO YA MICHAEL JACKSON YOU ARE NOT ALONE

😂😂😂😂😂😂

Refa wakike mrundi kwenda Cameroon

#Refa wakike mrundi Suavis IRATUNGA ameorodheshwa kwenye orodha ya warefa 11 wa kati watakao simamiya michuano ya 10 ya CAN yatakayo anza rasmi tarehe 19 Novemba hadi 3 Decemba 2016 nchini Cameroun . Kwenye jumla ya warefa 11 na warefa wapembeni 14 , mwanadada Suavis atakuwa ni balozi wa Burundi kwenye michuano hiyo. Fahamu yakwamba itakuwa mara yake ya kwanza kushiriki kwenye Kombe la Afrika ,ila alikuwa tayari kisha chezesha michuano kadhaa nchi mbali mbali kama Ethiopia , Guinea-Equator , Djibouti, Uganda kwenye Cecafa Women cup nakusimamiya fainali iliyo zipambanisha Tanzania na Uganda . Amejaliwa piya kuchezesha mechi nyingi kwenye ligi ya taifa nchini ,vile vile alibahatikiwa kupata mafunzo tiki tiki kwenye nchi tofauti kama Misri na kungineko.

N.B : Orodha kamili ipo hapo kwa hizo picha

Jiepushe

Ikiwa una kigugumizi ni vizuri ukajifunza kukwepa maneno ambayo yatakuletea matatizo,
kwa mfano yanaweza kukukosti ukiingia katika mgahawa ukaamua kuomba juisi ya matango,

pia ukimkuta Dem anauza matikiti, we pita tu usianze kusifu ukubwa wa matikiti hayo, ni kitu cha hatari.

Ukiwa una shida ya visa ya kwenda
Uchina,
wewe andika katika karatasi kuliko
kujaribu kueleza watu unaweza usieleweke.

Ni maneno mengi ambayo kwa kweli ningeweza kushauri lakini tuanzie na haya machache kwanza.

Huduma Ya Kwanza Kwa Mtu Aliyekula Au Kunywa Sumu

Mtu anaweza kula au kulishwa sumu katika mazingira mbalimbali. Kuna watu wengine huamua kujaribu kukatisha maisha yao kwa kunywa sumu kutokana na sababu mbalimbali za kimaisha. Lakini vyovyote iwavyo katika maisha yako au ya ndugu, jamaa na rafiki kukatisha maisha kwa kula au kunywa sumu sio suluhisho la kukimbia matatizo ya maisha bali ni kuingia kwenye matatizo makubwa mno kwani huko roho itakapokwenda ni MAJUTO MAKUU!

Endapo itatokea mtu amekunywa sumu au amekula chakula chenye sumu muwahishe hospitali au kituo cha afya haraka kama utaona hali hizi: kuwa na kichefuchefu, kutapika au kuharisha, damu kwenye kinyesi, kukosa mkojo, mate kuwa machache mdomoni na yenye mnato au macho kuingia ndani.

Wakati unafanya harakati za kumpeleka kwenye kituo cha afya, mpe tiba mojawapo ya hizi: Pia ukiona sumu sio kali sana maana mara nyingine tunaweza kula chakula lakini baada ya muda fulani tunasikia matumbo yanauma au tunaharisha,

Tumia tiba hizi:

Changanya siki aina ya 'Apple cider vinegar' kijiko cha chai (15ml) kwenye maji ya moto au vuguvugu kiasi cha kikombe kimoja (230ml) kisha mpe anywe. Rudia kila baada ya masaa 2 - 3.
Saga mkaa kisha chukua kiasi cha unga wa mkaa (500mg - 1g) changanya kwenye maji kikombe kimoja (230ml) mpe anywe. Rudia kila baada ya masaa 2- 3.

Kwa tumbo linalouma kutokana na sumu au chakula chenye sumu alichokula mtu anywe chai iliki au peppermint ili kutuliza tumbo. peppermint au iliki ni viungo vya vyakula vinavyopatikana sokoni au suppermarket. Apple cider vinegar ina matumizi mengi sana katika maisha yetu ya kila siku hivyo ni bidhaa muhimu kuwa nayo nyumbani kwako!

Le designer de la Coupe du monde Silvio Gazzaniga est mort

RIP Silvio Gazzaniga - the creator of the FIFA World Cup Trophy.

Il avait dessiné le nouveau trophée de la Coupe du Monde, remis pour la première fois en 1974.

L'Italien Silvio Gazzaniga (95 ans), connu pour avoir créé l'actuel trophée de la Coupe du monde, est décédé lundi. «Son» trophée avait remplacé en 1974 l'ancienne version du trophée Jules Rimet. Gazzaniga, qui avait également participé à la création des trophées de la Coupe de l'UEFA et de la Supercoupe de l'UEFA, a été salué par la planète foot, du président de la Fifa Gianni Infantino à Cafu.

10 ème journée English Premier League 16/17

Godillots de Lionel Messi

Frank de Boer afutwa Inter Milan baada ya siku 85

Frank de Boer amefutwa kazi na klabu ya Inter Milan ya Italia baada ya kufanya kazi kwa siku 85 pekee ambapo ambapo ameshindwa mechi nne ligini.

Inter wamo nambari 12 kwa sasa Serie A baada ya kushindwa 1-0 Sampdoria Jumapili.

Hiyo ilikuwa mechi yao ya nne kushindwa katika mechi tano za ligi walizocheza chini yake msimu huu.

De Boer, mwenye myaka 46, alikuwa beki wa Uholanzi enzi za uchezaji wake na aliwahi kuwa mkufunzi wa Ajax.

Alihusishwa na kuhamia klabu za Everton na Southampton majira ya joto.

Inter watakutana na Southampton ligi ndogo ya Ulaya, Europa League siku ya Alhamisi.

Mkufunzi wa timu ya vijana Stefano Vecchi atakuwa kwenye usukani mechi hiyo.

Wakati wa uchezaji wake, alichezea Ajax, Barcelona, Galatasaray na Rangers.

Lizer adai msanii yeyote anaweza kurekodi Wasafi Records

Ukizungumzia kati ya studio zenye hits nyingi kwa sasa huwezi kuacha kuitaja Wasafi records iliyo chini ya WCB lebo ambayo wanatokea wakali kibao kama Diamond, Rich Mavoko, Harmonize, Ray Vanny na wengine kibao.

Lakini imekuwa ni mara chache sana kusikia studio hiyo ikifanya kazi na wasanii wengine tofauti na hao niliowataja kama tunavyoona kwenye studio nyingine ukiwatoa Dully Sykes, Shetta pamoja na Chege ambao nao wanachukuliwa kama ni wana familia ya WCB.

Nikafika mpaka WCB nikapiga story na producer wa studio hiyo anayefahamika kwa jina la Lizer ambaye aliniambia kuwa Wasafi Records ni kama studio zingine na msanii yeyote anaweza kwenda kufanya kazi na studio hiyo.

“kama studio zingine wanavyofanya nasi tunafanya hivyo hivyo pia. Msanii mwingine yeyote kutoka sehemu yoyote anaruhusiwa kuja kurekodi hapa. Hatuna bei kubwa sana bei yetu ni ndogo sana ukizingatia na studio ilivyo kubwa lakini bei yetu ni ndogo sana,” alisema Lizer.

NA EDWARD FABIAN
Bongo

Schweinsteiger aandika ujumbe huu kwa mashabiki wa Man United

Baada ya kufanikiwa kurudishwa kuanza kufanya mazoezi kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United, Bastian Schweinsteiger ameandika ujumbe wa kuwatia moyo mashabiki wa timu hiyo.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, kiungo huyo ambaye ni raia wa Ujerumani ameandika, “Felt great today! Team is in good shape, results will follow! @manchesterunited.”

Mchezaji huyo amekuwa na wakati mgumu ndani ya timu hiyo chini ya kocha Jose Mourinho akiwa mpaka sasa hajacheza mechi hata moja tangu msimu ulipoanza mwezi Agosti, mwaka huu.

Mara ya mwisho nahodha huyo wa zamani wa Ujerumani kuchezea timu yake hiyo ya United ilikuwa ni msimu uliopita wa mwezi Machi, mwaka huu akiwa chini ya kocha Louis Van Gaal aliyetimuliwa.

Barua ya Tupac kuuzwa

Ni miaka 20 tangu afariki rapper mkongwe, Tupac. Na sasa barua ambayo aliiandika, mwenyewe inatarajiwa kuuzwa kwa kiasi cha $172,750 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 378 za kibongo.

Kampuni ya Goldin Auctions, imesema barua hiyo iliyondikwa na Tupac Shakur ni moja ya vitu kumi vilivyokuwa vikimilikiwa na rapper huyo ambavyo vyote vitauzwa kwa mtonyo wa $206,625.

Wachezaji 10 wanaolipwa mshahara mkubwa duniani, Afrika yupo mmoja

List mpya ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa duniani imetoka October 31 2016. Staa wa timu ya taifa ya Wales ambaye anaichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Gareth Bale ameingia katika TOP 3 ya wachezaji wa soka wanaolipwa pesa nyingi zaidi duniani ambapo ameingia katika list hiyo kutokana na mkataba wake mpya alio saini na Real Madrid.

Mchezaji kutoka Afrika yupo mmoja tu katika list hiyo, kiungo wa Man City na raia wa Ivory Coast Yaya Toure yupo nafasi ya 10 katika list ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa duniani.

Hii ndo list kamili