Alibaba

samedi 25 juin 2016

Mwanamke Mwenye Hedhi Afanye Nini Masiku Ya Mwisho Kupata Laylatul Qadr

Mwanamke Mwenye Hedhi Afanye Nini Masiku Ya Mwisho Kupata Laylatul  Qadr
 

SWALI:

Nilikuwa nawaza mwanamke mwenye hedhi afanye nini usiku wa Laylatul-Qadr ili aweze kupata thawabu zaidi kwa kujishughulisha na ibada? Na kama inafaa, ibada ya aina gani inaruhusiwa afanye usiku huo?

JIBU:

Alhamdulillah.

Mwanamke mwenye hedhi anaweza kufanya vitendo vyote vya ibada isipokuwa kuswali, kufunga, kuzunguka Ka'abah na kukaa I'itikaaf Msiktini.

Imesimuliwa kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  alikuwa akikesha usiku katika siku kumi za mwisho za Ramadhaan.

(Al-Bukhaariy 2401) na (Muslim 1174) wamesimulia kwamba Mama wa Waumini 'Aaishah رضي الله عنها amesema ((Zinapoingia siku kumi za mwisho katika Ramadhaan, Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hujiepusha na wake zake, na hukesha usiku na kuwaamsha 'aila (familia) yake))

Kukesha usiku haina maana kwamba ni kwa kuswali pekee, bali ni kwa kila aina ya vitendo vya ibada, na hivi ndivyo walivyofasiri Ma'ulamaa.

Al-Haafidh kasema: "Kukesha usiku ina maana kwamba kufanya aina za vitendo vya ibada"

An-Nawawy kasema:  "Kukesha usiku kwa kusimama kuswali na kadhalika",  akasema katika 'Awn al-Ma'abuud' kwamba ni kuswali, kufanya dhikr na kusoma Qur-aan.

Kuswali kwa kusimama ni kitendo bora kabisa Muislamu anaweza kufanya usiku wa Laylatul-Qadr kutokana na kauli ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم :((Yeyote atakayesimama  kuswali  usiku wa Laylatul-Qadr kwa imani na kutaraji malipo atafutiwa madhambi yake ya nyuma)) Al-Bukhaariy 1901 na Muslim 760

Kwa sababu mwanamke mwenye hedhi haruhusiwi kuswali, ila anaweza kukesha usiku kwa kufanya aina ya vitendo vya 'Ibaadah zingine mbalimbali kama vile:

1) Kusoma Dhikr

2) Dhikr kama kusema Subhaan-Allaah, La ilaaha illa Allaah, al-Hamdu Lillaah, anaweza kurudia kusema Subhaana-Allaah wal-Hamdu Lillaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar na vile vile Subhaana Allaah wa bihamdihi, Subhaana Allaahul-‘Adhiym.

3) Istighfaar kwa kurudia kusema "Astaghfiru-Allaah"

4) Kuomba Du'aa.  Anaweza kumuomba Allaah anayohitaji ya duniani na Akhera kwani Du'aa ni kitendo bora kabisa cha 'Ibaadah. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema ((Du'aa ni 'Ibaadah))  At-Tirmidhiy, 2895; na imesemwa kuwa ni  Swahiyh na Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy, 2370

Mwanamke mwenye hedhi anaweza kufanya vitendo vyote hivi usiku wa Laylatul-Qadr.

Tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atusaidie kuweza kufanya yale Anayoyapenda na Yanayomridhisha.  Na tunamuomba Atutakabalie vitendo vyetu vyema.

samedi 11 juin 2016

UTAFITI KWA WANAUME WA AFRIKA

UTAFITI KWA WANAUME WA AFRIKA!

1. Wanaume wakatili zaidi Afrika - Waangola, Warundi na Wanubi (Sudan). Ukiwakosea ni kipigo au kifo. Kwao hakuna msamiati uitwao "MSAMAHA".

2. Wanaume wanaojali zaidi familia zao Afrika - WASENEGAL.

3. Wanaume wanaopigwa zaidi na wake zao - WAKENYA.
(Kati ya wanaume 10 nchini Kenya 7 wanapokea kipigo kutoka kwa wake zao. Chama cha kutetea haki za wanaume hadi sasa kina wanachama laki 8).

4. Wanaume wanaosali zaidi Afrika - WASOMALI.
(kati ya wanaume 10 wa kisomali, 8 huswali swala 5 kila siku. Hata katikati ya vita huwaachi kuswali).

5. Wanaume matapeli zaidi Afrika - WANIGERIA (kati ya wanaume 10 wa Nigeria, 6 ni matapeli wa kutupwa. Hata kama ni Askofu ukijilengesha anakutapeli tu).

6. Wanaume wanaopenda dezo na kulelewa zaidi Afrika - WAKONGO (hawa wakioa mwanamke mwenye pesa huhamia kwa mke. Wanaitwa "MARIO").

7. Wanaume wasomi zaidi Afrika -WASHELISHELI (SYCHELLES). (Kila wanaume 100, 40 wana degree. Tanzania kila wanaume 100 ni watatu wana degree).

8. Wanaume washamba zaidi Afrika - WAERITREA.
(Ukienda kanisani/msikitini na gari jipya wanaahirisha kusali washangae gari kwanza).

9. Wanaume wachawi na Washirikina zaidi Afrika - WAGAMBIA.
(Rais wao YAHYA JAMMEH hutumia waganga na wapiga ramli kama sehemu ya walinzi wake).

10. Wanaume wenye mikwara mingi mdomoni lakini waoga kutake "action" - WATANZANIA.

vendredi 10 juin 2016

TUSOMENI Qor'an by The Light of Peace

Écouter TUSOMENI Qor'an by The light of Peace.mp3 par Abuchief Djuma #np sur #SoundCloud https://soundcloud.com/abuchief-djuma/tusomeni-qoran-by-the-light