Google tag

dimanche 18 septembre 2016

Jose Mourinho amtetea Pogba kwa kiwango chake

Jose Mourinho amemkingia kifua kwa watu wanaombeza Paul Pogba ambaye ndiye mchezaji ghali duniani kwa sasa kutokana na dau alilonunuliwa kwenye dirisha la usajili la paundi milioni 89.

Mchezaji huyo amekuwa akitupiwa lawama kwenye mechi za hivi karibuni baada ya timu yake ya Manchester United kupoteza mechi mbili mfululizo ikiwemo moja ya ligi waliyofungwa Na Manchester City na nyingine ya Europa waliyofungwa katikati ya wiki hii na Feyenoord.
Mourinho amesema kuwa anajua kuwa Pogba ni mchezaji mzuri na atakuwa kwenye kiwango kizuri muda siyo mrefu.

“I just want Paul to forget that and to play his football He had Euros, no pre-season then holidays and then came back He had a very good impact in the first game but it’s normal after the first game.,”
amesema Mourinho.

“He has a little decrease But I am full of trust with him because I know the player he is I know he is a very good guy with a lot of ambition so the form will come naturally with the team improving. The team improves, he will improve. No problem.”

Aidha kocha huyo ameongeza kuwa watu wasijadili kuhusu fedha aliyonunuliwa mchezaji huyo kwa kuwa ni fedha ya kawaida sana.