Google tag

samedi 15 avril 2017

Wema Sepetu, Gabo kuwasha moto kwenye filamu ‘Heaven Sent’

Malkia wa filamu Wema Sepetu pamoja na Gabo Zigamba wataonekana kwenye filamu mpya ‘Heaven Sent’ inayoongozwa na Neema Ndepanya chini ya kampuni ya Fontana Entertainment.

Katika filamu hiyo Wema atakuwa kwenye mahusiano na Gabo Zigamba.
“Sometimes in Life, You meet people for a Reason…. Im so happy I found the Reason I met you Gabo Zigamba #TheMaking of #HeavenSent,” aliandika Wema Instagram akiwa katika maandalizi ya kazi hiyo.

Aliongeza, “Msichana naona mpaka mwaka kuisha watanzania watakuwa wameshaona uwezo wangu wa kubadilika wenye character tofauti. Nashukuru maana mpaka uchizi umenichezesha. Nashkuru sana binti Ndepanyaa.,”

Stori pamoja na script ya filamu hiyo imeandaliwa na Neema Ndepanya.

Hatma ya Arsenal kuhusu Big 4

Arsenal inakabiliwa na changamoto kubwa kufuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya kulingana na mkufunzi wa klabu hiyo Arsene Wenger ambaye ameongezea kuwa hakuna kilichobadilika kuhusu hatama yake ya siku zijazo.
Kushindwa kwao kwa 3-0 na Crystal Palace kuliiwacha klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya sita ,na ponti saba nyuma ya klabu ya Manchester City iliopo katika nafasi ya nne huku ikiwa imesalia mechi nane pekee.

Wenger ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu ameiongoza Arsenal katika nafasi nne bora za ligi hiyo katika miaka 20 aliyokuwa mkufunzi wake.
Kuhusu timu nne bora, alisema: ''Tunaweza kuwa katika timu nne bora au la''.

Raia huyo wa Ufaransa amepewa ombi la kandarasi ya miaka miwili ijapokuwa hajatangaza iwapo ataendelea au la.
Kushindwa kwao kwa mechi tano kati ya 10 katika mechi za ligi kuu kumewafanya mashabiki wa Arsenal kumtaka Wenger kuondoka katika klabu hiyo.
Alipoulizwa kuhusu hatma yake ya baadaye alisema: kile kitakachoamuliwa na bodi hakinihusu mimi.
''Ninafanya kile nilichoajiriwa kufanya, mchezo mzuri wa timu na kile mashabiki wanachotaka ambacho ni timu iweze kucheza vyema''.

The Gunners watacheza dhidi ya Middlesborough siku ya Jumatatu.
Wenger amekataa kujibu madai kwamba mshambuliaji Alexis Sanchez amepewa kandarasi mpya ya £300,000 kwa wiki.