Marekani imesema kuwa imemuorodhesha mwana wa mwisho wa Osama Bin laden Hamza katika orodha ya magaidi wanaosakwa na taifa hilo.
Idara ya maswala ya kigeni imesema kuwa hamza Bin Laden ameanza kushiriki katika maswala ya kundi la al Qaeda ,kundi la jihad lililofadhiliwa na babake.
Amesema kuwa atalipiza kisasi mauaji ya babake yaliotekelezwa na kikosi maalum cha Marekani kwa kutekeleza mashambulizi dhidi ya Wamarekani.
Sasa atapigwa marufuku kwa kufanya biashara na raia wa Marekani huku mali yake ikipigwa tanji.
Mkuu wa kitengo cha usalama cha kundi la al-Qaeda Ibrahim al-Banna pia ameongezwa katika orodha hiyo .
Marekani imetoa kitita cha dola milioni 5 kwa mtu yeyote atakayemkamata al-Banna.