Msanii mashuhuri wa filamu nchini Ukraine, Pasha Lee aliyeamua kuweka sanaa pembeni na kuingia vitani kuipigania nchi yake, ameuawa baada ya kupigwa na makombora ya Urusi katika Mji wa Irpin ambako mashambulizi makali yanaendelea.
Pasha aliyefariki akiwa na umri wa miaka 33, alipata umaarufu mkubwa kutokana na kazi yake ya uigizaji na utangazaji ambapo filamu za Lion King na Hobbit, zilimfanya apate umaarufu ndani na nje ya nchi hiyo.
Siku tano kabla ya mauti yake, staa huyo ambaye ni mzaliwa wa Crimea, aliposti picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa amevaa mavazi ya kijeshi na kusindikiza na maneno ya 'LET'S UNITE' akiwataka wananchi wa Ukraine kuungana kupambana na uvamizi wa Urusi.