Alibaba

dimanche 30 avril 2017

INTER HAVE FINANCIAL MUSCLE TO SIGN MESSI, CLAIMS MAZZOLA

Inter have financial muscle to sign Messi, claims Mazzola

Inter boast the financial power to sign Lionel Messi from Barcelona, former Nerazzurri star Sandro Mazzola has said.

There has been speculation for some months that the Serie A side, bankrolled by their Suning Holdings Group owners, could try to sign Messi with a stunning transfer bid at the end of the season.

Former Inter president Massimo Moratti said in January the club are planning to sign a global superstar before next season, although he rejected the suggestion that Messi is their top target.

But Mazzola, a double European champion as part of the famous Inter side of the 1960s, believes Suning's backing makes Messi at San Siro a very real prospect.

"Suning have the strength to get those they want, including Messi," he told Il Mattino.

To read full article - https://goo.gl/AY3ByW

Sunderland kupoteza nafasi ya kubaki Premier League

Kipindi cha miaka kumi cha klabu ya Sunderland katika ligi ya Uingereza hatimaye kimekwisha baada ya kushindwa na Bournemouth nyumbani.
Matokeo hayo pamoja na yale ya sare kati ya Hull City na Southampton yanamaanisha timu hiyo ya David Moyes ina pointi 14 ikiwa imesalia mechi nne.

Joshua King wa Bournemouth alifunga bao la pekee ikiwa imesalia dakika 2 na kuipa ushindi timu yake.
Raia huyo wa Norway pia karibu afunge katika dakika ya 20 lakini shambulio lake lilipiga mwamba wa goli na kurudi katika mikono ya kipa Pickford.

Hiyo ni mara ya 23 ya Sunderland kupoteza ,hatua inayomaanisha timu hiyo ya Black Cat imeshushwa dajara kutoka ligi ya Uingereza kwa mara ya nne.

jeudi 20 avril 2017

Uefa Champions League semi-finalists 2017

UCL semi-finalists

Siku ambayo BBC ilikosa habari za kutangaza

Siku hizi ni vigumu sana kutafakari hali ilivyokuwa kabla ya mafanikio makubwa kupatikana katika teknolojia ya mawasiliano.

Imekuwa kama ada kwamba kila wakati lazima kuwe na habari.
Lakini zamani, hali ilikuwa tofauti kabisa.
Miaka 87 iliyopita, mnamo 18 Aprili 1930, msomaji wa habari katika BBC alikosa cha kutangaza.

Taarifa aliyoisoma wakati wa taarifa ya habari ya saa tatu kasorobo usiku ilikuwa: "Hakuna habari".

Baadaye, kinanda kilichezwa kwa dakika 15 zilizosalia ambazo zilikuwa zimetengewa habari.

Baadaye, matangazo yalipelekwa Ukumbi wa Malkia katika jumba la Langham Place, London ambapo kulikuwa na tamasha la muziki wa Wagner.

Miaka 87 baadaye, hali ni tofauti kabisa. Jumanne ilikuwa siku iliyojaa habari tele.
Watu walipokuwa wanashiriki pilkapilka za hapa na pale baada ya Pasaka, Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May aliitisha kikao saa tano mchana na kuahidi kutoa tangazo muhimu.

Wengi walianza kutafakari tangazo lake lingekuwa nini - hadi pale alipotangaza mpango wa kuitisha uchaguzi wa mapema tarehe 8 Juni.

Kulikuwa pia na mzozo kati ya Marekani na Korea Kaskazini ambao umekuwa ukitokota kwa wiki kadha sasa.
Kulikuwa pia na maadhimisho ya uhuru wa Zimbabwe ambapo kiongozi wa muda mrefu wa taifa hilo Robert Mugabe aliwahimiza raia kuutetea na kuulinda uhuru huo.

Nchini Ufaransa, mmoja wa wagombea wakuu katika uchaguzi wa urais Marine le Pen alisema atazuia wahamiaji kuingia nchini humo iwapo atashinda uchaguzi
Siku hizi, BBC ina wafanyakazi wengi na uwezo mkubwa wa kukusanya habari tofauti na hali ilivyokuwa 1930.

Kumekuwa pia na mabadiliko ya maana ya habari.
Wakati huo, habari nyingi zilitoka kwa mashirika ya habari ya kimataifa na matangazo ya serikali.
Siku hizi, watu wa kawaida wanaweza kuwa mada ya habari.

Wakati huo, watangazaji walikuwa pia hawafahamiki na wasikilizaji.
Siku hizi, wengi wa watangazaji wanafahamika sana na hata ni watu mashuhuri.

mercredi 19 avril 2017

UEFA: Real Madrid yailaza Bayern Munich 4-2 Ligi ya Mabingwa Ulaya

Cristiano Ronaldo alifunga mabao matatu na kuwawezesha mabingwa watetezi wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Real Madrid kuwatimua Bayern Munich kutoka kwenye michuano ya msimu huu katika hatua ya robofainali.
Mechi hiyo iliyomalizika 4-2 hata hivyo ilijaa utata na mshindi alipatikana katika muda wa ziada.

Kiungo wa kati wa Bayern Munich Arturo Vidal alitimuliwa uwanjani dakika ya 84 jambo ambalo lilionekana kuathiri mwelekeo wa mechi hiyo.
Ronaldo naye alionekana kuwa alikuwa ameotea alipokuwa anafunga bao la pili la Real muda wa ziada.
Bayern, ambao walihitaji mabao mawili kusonga, alikuwa wameongoza kupitia penalti iliyofungwa na Robert Lewandowski.

Madrid walitatizika kutamba kwenye mechi hiyo iliyochezewa Bernabeu kabla ya Ronaldo kufunga kwa kichwa kutokana na krosi ya Casemiro.
Bayern walijibu sekunde 36 baadaye Sergio Ramos alipojifunga na kulazimisha mechi hiyo kuingia muda wa ziada.
Ni hapo ambapo Ronaldo alifunga bao la utata la Madrid.
Nahodha huyo wa Ureno kisha alifunga la tatu - lake la 100 katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Marco Asensio aliwakamilishia ushindi kwa kuongeza la tatu.

Madrid watamfahamu mpinzani wao nusufainali wakati wa droo Ijumaa.
Majirani wao Madrid Atletico Madrid walisonga kwa kuwaondoa Leicester City.
Kwenye robofainali hizo nyingine, Barcelona wanakutana na Juventus nao Monaco wakutane na Borussia Dortmund baadaye Jumatano.

Mashabiki wamrushia panya mchezaji nchini Denmark

Mechi ya ligi kuu ya Denmark kati ya Brondby na FC Copenhagen ilitibuka baada ya mashabiki kuwarushia panya waliokufa uwanjani.
Mashabiki wa Brondby walimrushia panya mlinzi wa Copenhagen Ludwig Augustinsson alipokwenda kupiga kona.

Copenhagen ilishinda mechi hiyo 1 - 0 na sasa ni wa kwanza huku ikiishindia timu ya pili ambayo ni Brondby kwa alama 13.
"Sio vyema kuwa na baadhi ya wageni ambao hawawezi kuwa na tabia njema," alisema mkurugenzi wa michezo wa Brondby, Troels Bech.

Video iliyorekodi yaliyotokea uwanjani inaonyesha mchezaji wa Slovenia Benjamin Verbic akimsaidia mwenzake Augustinsson kuwatoa angalau panya wawili kutoka uwanja huo wa Brondby ambao unaweza kubeba mashabiki elfu 28.
Brondby ni mabingwa mara 10 wa Denmark na FC Copenhagen inayosimamiwa na aliyekuwa meneja wa Wolverhampton Wanderers Zamani Solbakken, wameweza kunyakua ushindi mara 11

samedi 15 avril 2017

Wema Sepetu, Gabo kuwasha moto kwenye filamu ‘Heaven Sent’

Malkia wa filamu Wema Sepetu pamoja na Gabo Zigamba wataonekana kwenye filamu mpya ‘Heaven Sent’ inayoongozwa na Neema Ndepanya chini ya kampuni ya Fontana Entertainment.

Katika filamu hiyo Wema atakuwa kwenye mahusiano na Gabo Zigamba.
“Sometimes in Life, You meet people for a Reason…. Im so happy I found the Reason I met you Gabo Zigamba #TheMaking of #HeavenSent,” aliandika Wema Instagram akiwa katika maandalizi ya kazi hiyo.

Aliongeza, “Msichana naona mpaka mwaka kuisha watanzania watakuwa wameshaona uwezo wangu wa kubadilika wenye character tofauti. Nashukuru maana mpaka uchizi umenichezesha. Nashkuru sana binti Ndepanyaa.,”

Stori pamoja na script ya filamu hiyo imeandaliwa na Neema Ndepanya.

Hatma ya Arsenal kuhusu Big 4

Arsenal inakabiliwa na changamoto kubwa kufuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya kulingana na mkufunzi wa klabu hiyo Arsene Wenger ambaye ameongezea kuwa hakuna kilichobadilika kuhusu hatama yake ya siku zijazo.
Kushindwa kwao kwa 3-0 na Crystal Palace kuliiwacha klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya sita ,na ponti saba nyuma ya klabu ya Manchester City iliopo katika nafasi ya nne huku ikiwa imesalia mechi nane pekee.

Wenger ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu ameiongoza Arsenal katika nafasi nne bora za ligi hiyo katika miaka 20 aliyokuwa mkufunzi wake.
Kuhusu timu nne bora, alisema: ''Tunaweza kuwa katika timu nne bora au la''.

Raia huyo wa Ufaransa amepewa ombi la kandarasi ya miaka miwili ijapokuwa hajatangaza iwapo ataendelea au la.
Kushindwa kwao kwa mechi tano kati ya 10 katika mechi za ligi kuu kumewafanya mashabiki wa Arsenal kumtaka Wenger kuondoka katika klabu hiyo.
Alipoulizwa kuhusu hatma yake ya baadaye alisema: kile kitakachoamuliwa na bodi hakinihusu mimi.
''Ninafanya kile nilichoajiriwa kufanya, mchezo mzuri wa timu na kile mashabiki wanachotaka ambacho ni timu iweze kucheza vyema''.

The Gunners watacheza dhidi ya Middlesborough siku ya Jumatatu.
Wenger amekataa kujibu madai kwamba mshambuliaji Alexis Sanchez amepewa kandarasi mpya ya £300,000 kwa wiki.