Mchezaji wa klabu ya Chelsea Eden Hazard ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba katika EPL, huku tuzo ya kocha bora mwezi Oktoba ikienda kwa kocha wa Chelsea, Antoine Conte ambaye ameshinda tuzo ya kocha bora wa EPL.
Chelsea imeshinda mechi zote 4 za ligi kuu katika mwezi huo, wakifunga magoli 11 na hawakuruhusu kufungwa goli hata moja, huku mchezaji Hazard akiwa amecheza mechi 4,akifunga goli 3 na kutoa Assist 1.