Labda una ndoto za kuwa
mtayarishaji wa filamu mbalimbali hapo baadaye, au siyo? Au unataka
kuweka rekodi kwa kutengeneza filamu nzuri ambazo zitakuja kukimbiza
sana Tanzania na duniani kote, au siyo? Basi unaweza kutazama baadhi ya
picha, kidogo unaweza kugundua wenzetu wanafanyaje mpaka filamu
kukamilika.
Wenzetu wameendelea, mpaka kufika hapo
walipokuwa, haikuwa miujiza, haikuwa bahati, ni kwamba walijipanga,
walisoma mpaka kufika hapo walipokuwa.
Ni safari ndefu, yenye kukatisha tamaa
lakini mwisho wa siku wakafanikiwa. Wakaanza kutengeneza filamu nzuri,
zenye mazingira ya kupendeza mpaka wewe mwenyewe ukazipenda.
Hebu tazama baadhi ya picha za filamu,
wanavyoigiza na baadaye kipande kuingizwa kwenye kompyuta na kuanza
kutengenezwa. Hakika utazipenda hizi picha.