Alibaba

dimanche 30 juin 2013

danse sexy

RIHANNA ANIKA NYETI ZAKE KWA MARA NYINGINE TENA.. ...

RIHANNA ANIKA NYETI ZAKE KWA MARA NYINGINE TENA.. ...:
Hii ni  makusudi au ni bahati mbaya, msanii kutoka nchini marekani ambaye ni rihanna amekua katika aibu nzito siku za hivi karibuni baada ya picha yake ya mara ya kwanza kuonesha nyeti yake, leo hii picha ya msanii huyo ambayo imeonyesha live maungo yake (nyeti) wakati alipokua beach..., hapana chezea mapaparazi..

mercredi 26 juin 2013

MASKINI MZEE MANDELA... DAKIKA ZAKE 40 ZA HATARI

Johannesburg, Afrka Kusini
AFYA ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ‘Madiba’ ni mtihani tata kwa ikulu ya nchi hiyo, hivi karibuni, iliingia kwenye skendo kwamba ilifanya uzembe uliokaribia kusababisha kifo cha mzee huyo mwenye umri wa miaka 94.
Nelson Mandela ‘Madiba’.
Habari hizo ambazo awali zilifanywa siri kabla ya kuvuja wikiendi iliyopita, zinasema kuwa Ikulu ya Afrika Kusini ilikosa umakini, hivyo ikaacha gari bovu limbembe Mzee Mandela na matokeo yake lilizimika kwenye barabara kuu (high way).
Kuzimika kwa gari hilo, kulisababisha hekaheka lakini ufumbuzi wa haraka ulikosekana mpaka dakika 40 baadaye ndipo ‘ambulance’ nyingine ilipofika eneo la tukio, ikambeba Mzee Mandela na kumuwahisha hospitali.
Ikulu ya Afrika Kusini imelazimika kutoa tamko, baada ya wachambuzi kuelezea tukio hilo kwamba zilikuwa dakika 40 za hatari za Mzee Mandela, kwa maana nusura zichukue uhai wa kiongozi huyo aliyeongoza vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, miaka ya 1900 nchini humo.
Tukio lenyewe, lilijiri Juni 8, mwaka huu (zaidi ya wiki mbili zilizopita) lakini ikawa kimya katika vyombo vya habari, japo minong’ono iliendelea kushamiri, kabla ya mambo kuwekwa hadharani wikiendi iliyopita.

KIVIPI DAKIKA 40 ZA HATARI?
Kwa mujibu wa habari pamoja na makala za wachambuzi mbalimbali wa kisiasa nchini Afrika Kusini, muda mfupi baada ya Mzee Mandela kuondolewa barabarani pale gari lilipomzimikia na kuwahishwa katika Hospitali ya Mediclinic Heart, Pretoria, uvumi ulienea kuwa ameshafariki dunia.
Mchambuzi wa siasa za Afrika Kusini, Olwethu Sipuka ambaye makala zake hupatikana zaidi kwenye Tovuti ya Politicweb ya nchini humo, alieleza kuwa zile dakika 40 zilikuwa za hatari mno kwa Mzee Mandela ndiyo maana wananchi waliamini uvumi kuwa alifia pale.
“Afadhali taarifa za gari lililomzimikia zilisambaa baadaye, kama zingewahi, wananchi wangekusanyika eneo la tukio na pengine ingekuwa hatari sana kwa afya ya Madiba,” aliandika Sipuka na kuongeza:
“Kama wananchi wangewahi kufika pale barabarani, pengine wangetaka kumbemba Madiba wampeleke hospitali. Kama wangeamini amekufa, isingekuwa rahisi kwao kukubali ambulance nyingine imbembe. Hiyo ni hatari ambayo ingeweza kumsababishia kifo.”
Kwa upande mwingine, habari zinasema kuwa baada ya gari kuzimika, Mzee Mandela hakupata huduma yoyote kwa muda wote wa dakika 40 ambazo alikwama pale barabarani.
Dk. Mamphela Ramphele ambaye naye ni mchambuzi wa siasa za nchi hiyo, alihoji katika makala yake ni kwa nini baada ya kuzimika ambulance ambayo ni ya kijeshi, haikwenda nyingine ya serikali kumchukua Mzee Mandela, badala yake ikaenda ya kiraia?
Aliandika kuwa afya ya Mzee Mandela haipaswi kufanyiwa mchezo, kwani jeshi la Afrika Kusini halina ambulance moja, ile ya kiraia haiwezi kuwa na ubora unaotoa huduma kwa mgonjwa anayestahili matibabu ya ICU (kiwango cha uangalizi wa hali ya juu).
Zipo taarifa zinazosema kuwa zile dakika 40 alizokwama barabarani, zilisababisha hali ya Mzee Mandela iwe mbaya zaidi, kwani baada ya ambulance ya pili kuwasili, aliwekwa katika mashine ya oksijeni ambayo ilimsaidia kupumua mpaka alipofikishwa hospitali.
Mchambuzi mwingine, Blade Nzimande, aliandika kuwa kutoka Johannesburg, nyumbani kwa Mzee Mandela mpaka Pretoria kwenye Hospitali ya Mediclinic Heart, ni umbali wa zaidi ya maili 31 (kilometa 50) hivyo ilihitajika umakini wa hali ya juu.
“Alitolewa nyumbani akiwa na hali mbaya, inafahamika macho yote ya wananchi wa Afrika Kusini yanafuatilia mwenendo wa afya yake. Gari lililombemba halikutakiwa kuwa na hitilafu ya injini. Kuna uzembe mkubwa umefanyika.”   

IKULU YATOA TAMKO
Kutokana na kuenea kwa uvumi huo, Ikulu ya Afrika Kusini, wikiendi iliyopita, ilitoa tamko kuhusiana na tukio hilo la ambulance iliyokuwa imembeba Mzee Mandela kuzimika barabarani.
Msemaji wa Ikulu ya Afrika Kusini, Mac Maharaj, alisema kuwa ni kweli kwamba gari lililokuwa limembeba Mzee Mandela lilizimika barabarani lakini halikumwathiri kwa chochote.
“Alikuwa na madaktari ambao walijiridhisha kwamba hakutakuwa na hatari yoyote katika kusubiri gari lingine la kumpeleka hospitali,” alisema Maharaj kwa niaba ya Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.
Aliongeza: “Ambulance iliyokuwa imembeba ilikuwa inasindikizwa na magari mengine, kwa hiyo kama hali ingekuwa mbaya zaidi, angehamishwa katika gari lingine na kukimbizwa hospitali. Haikuonekana hatari kubwa.
“Timu ya madaktari kutoka idara ya ulinzi ilijiridhisha kwamba afya ya Mzee Mandela itakuwa salama ndiyo maana waliruhusu subira hiyo ya dakika 40. Ile ambulance ni ya jeshi, tulipewa taarifa baada ya kuzimika, tukafanya juu chini kupata nyingine, ikaonekana itachelewa zaidi ndiyo maana ikatumika ya kiraia.
“Tunapenda wananchi wote wajue kuwa tupo makini na afya ya mzee wetu. Ile ambulance ya kijeshi ina vifaa vyote ya ICU na madaktari waliokuwa wamemzunguka ni madaktari bingwa, kwa hiyo wana uwezo mkubwa. Hakukuwa na uzembe hata kidogo.”

ZUMA IKULU HAPAKALIKI
Kwa mujibu wa taarifa za Ikulu ya Afrika Kusini, afya ya Mzee Mandela, inasababisha Rais Zuma asiwe na utulivu, kwani muda mwingine anafuatilia maendeleo ya kiongozi huyo aliyewahi kufungwa jela miaka 27, kipindi anaongoza harakati za kupinga sera za ubaguzi wa rangi nchini humo.
Imeelezwa kuwa tangu Aprili 29, mwaka huu, pale Zuma alipomtembelea Mzee Mandela na kuona ukweli jinsi afya yake inavyobadilika na kuwa mbaya zaidi, amekuwa hakai akatulia ikulu, badala yake hutumia muda mwingi kufuatilia maendeleo ya rais huyo wa kwanza Mwafrika nchini Afrika Kusini.
Habari zinafafanua kuwa siku hiyo, Zuma ambaye aliongozana na viongozi wengine wa Chama cha African National Congress (ANC), kwenda kumjulia hali hali, alishtushwa kuona Mzee Mandela akiwa hatikisi kichwa wala kupepesa macho.
Chanzo kimoja kutoka Ikulu ya Afrika Kusini ambacho hakikutajwa jina, kilieleza kwamba hata safari za nje, Zuma amezipunguza kwa hoja kwamba taifa halitamwelewa yeye kuwa mbali katika kipindi hiki ambacho Mzee Mandela anaumwa sana, japo afya yake inaelezwa kuimarika.

MBEKI AWATOA HOFU WANANCHI
Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, amewatoa hofu wananchi wa nchi hiyo kuwa Mzee Mandela anaendelea vizuri, ingawa katika siku za hivi karibuni amekuwa akipelekwa hospitali mara kwa mara kwa ajili ya kutibiwa.
Mbeki aliyemrithi Mandela mwaka 1999, alisema kuwa ni vizuri wananchi wakadumisha sala kwa kumwombea mzee huyo badala ya kukata tamaa na kuamini uvumi kwamba ameshafariki dunia.

ANC YATAKA MANDELA AHESHIMIWE
Chama cha ANC, Jumamosi iliyopita, kilitoa tamko kuwa Mzee Mandela inabidi aheshimiwe na kwamba siyo kila mtu anaweza kuwa msemaji wa maendeleo ya afya yake.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Ikulu ya Afrika Kusini inabidi ifanye kazi vizuri kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za kweli na zenye uhakika kuhusu kiongozi huyo aliyeiongoza nchi hiyo kuanzia mwaka 1994 mpaka 1999.
“Chama chetu cha The African National Congress kwa mara nyingine kinataka pande zinazohusika zifanye kazi yake. Vilevile tunataka vyombo vya habari na familia, kuheshimu taarifa za faragha kuhusu Mandela.”

TATIZO NI MAPAFU
Mzee Mandela ambaye mwezi ujao anatarajiwa kutimiza umri wa miaka 95, kwa muda mrefu sasa anasumbuliwa na tatizo la mapafu kujaa maji.
Habari zinasema kuwa tatizo la mapafu, ni matokeo ya athari alizozipata akiwa gerezani kipindi alipofungwa miaka 27 jela katika miaka ya 1900.

TUMUOMBEE MZEE MANDELA
Mandela amekuwa kielelezo chema siyo tu kwa Afrika Kusini, bali Afrika na duniani kote. Nasi Watanzania kila mtu kwa imani yake ni vema kumuombea salama ili Mungu ampe nafuu na kumponya maradhi yanayomsibu kwa sasa.

UJIO WA OBAMA KUFURU

Na Mwandishi Wetu
UJIO wa Rais wa Marekani, Barack Obama ni kufuru tupu, kiasi cha fedha ambacho kinachotumika kugharamia ziara yake peke yake kinazidi mara mbili ya kile kilichoteketea pale mtangulizi wake, George W. Bush, alipotembelea nchini mwaka 2008.
Rais wa Marekani, Barack Obama.
Obama, rais wa kwanza mwenye asili ya Bara la Afrika kutawala Marekani, atawasili nchini Julai Mosi, mwaka huu na kufanya ziara ya siku mbili.
Inaaminika kuwa Bush alipokuja nchini, msafara wake uliigharimu Marekani kiasi cha dola milioni 50 (shilingi bilioni 80) lakini Obama na timu yake watatumia mara mbili ya hapo, yaani dola milioni 100 (shilingi bilioni 160).
Hesabu hiyo, ilimtisha hata Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohamed Dewji ‘Mo’ ambaye aliandika kwa mshangao katika akaunti yake ya Twitter, Jumamosi iliyopita: “Ujio wa Obama Tanzania utaigharimu Marekani dola milioni 100.”
UKUBWA WA MSAFARA
Kwa mujibu wa ziara mbalimbali ambazo Obama alishazifanya tangu alipoingia madarakani Januari 2009, msafara wake huwa na watu zaidi ya 800.
Obama ambaye ni Rais wa 44 wa Marekani, akiwa na mkewe, Michelle, huongozana na watu 500 ambao ni watumishi wa kawaida wa Ikulu ya Marekani, White House.
Katika wahudumu hao 500, wapo madaktari sita pamoja na wauguzi wengine zaidi ya 30, wapishi na kadhalika.
Msafara wa Obama, haukamiliki bila walinzi karibu 300 ambao jukumu lao huwa ni kumlinda rais huyo kwa ukaribu zaidi.
Kutokana na hesabu hiyo ni wazi kuwa Tanzania itakuwa na msukosuko wa aina yake pale Obama atakapowasili Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Hata hivyo, kwa vile ndege ya Rais wa Marekani, Air Force One, haina uwezo wa kubeba idadi hiyo ya watu, wengi wao watawasili kwa mafungu wiki hii ili kufanya maandalizi ya ujio wake.
Ulinzi wa Obama.
MASHUSHUSHU KILA KONA
Kuelekea siku ya ujio wa Obama, Jiji la Dar es Salaam, limeshawekwa chini ya ulinzi, mashushushu kutoka Marekani wametanda kila kona kuhakikisha rais huyo hapatwi na zahama yoyote akiwa nchini.
Maofisa wa CIA (Central Intelligence Agency) ambao kiuhalisia ndiyo Idara ya Usalama wa Taifa la Marekani, wanadaiwa kuwepo nchini tangu Januari, mwaka huu, lengo likiwa ni kuratibu na kuhakiki usalama wa nchi.
Vilevile inadaiwa, makomandoo wapatao 400 kutoka Taasisi ya Upelelezi ya Marekani, FBI (Federal Bureau of Investigation), waliwasili nchini kwa mafungu kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, jukumu lao likiwa ni kuweka mambo sawa.
Madai hayo yanajengwa na hoja kwamba hata pale FBI walipojitolea kutoa mchoro wa mtu aliyedaiwa kumpiga risasi na kumuua Padri Evarist Mushi, Machi mwaka huu, ilikuwa ni kwa haraka sana.
“Wale FBI walikuwa hapahapa Tanzania ndiyo maana walijitolea kutoa mchoro wa Padri Mushi kwa haraka sana, ingekuwa wapo Marekani wasigejitolea haraka vile.
“Sema sasa ilikuwa siri kubwa. Taarifa za ujio wa Obama kuja zipo tangu mwaka jana ila zilifanywa siri kwa sababu za kiusalama,” alisema ofisa mmoja wa Ikulu ya Tanzania kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.
Gari la Obama.
ANAKUJA NA MAGARI 21
Kwa mujibu wa taarifa za ziara za Rais  Obama, kiongozi huyo husafiri na jumla ya magari 21.
Obama husafiri na gari lake binafsi kama Rais wa Marekani aina Limousine Cadillac, ambalo halilipuki wala kuharibika hata likipigwa na bomu.
Gari hilo likilipuliwa na bomu, matairi peke yake ndiyo huungua lakini hubaki na rimu ambazo hutembea kwa umbali wa kilometa 500 bila wasiwasi.
Limousine Cadillac ambalo ni toleo maalum la mwaka 2009 kwa ajili ya Obama pekee, huambatana na magari mengine 20.
Kutokana na tafsiri hiyo, Obama akiwa nchini, atakuwa na msafara wake uliokamilika na unaojitegemea kwa asilimia 100.

MAGARI 21 YATAKUJA VIPI?
Habari zinasema kuwa Limousine Cadillac ndilo litakalokuja na Air Force One, Julai Mosi, mwaka huu, mengine 20 yatawasili kabla ya ujio wa Obama.
Inaelezwa kuwa sababu ya magari hayo 20 kutokea Marekani ni kwamba utaratibu wa White House unaeleza kuwa msafara wa Rais wa Marekani ndani ya nchi unapaswa kufanana na wowote ule anapokuwa nje ya nchi.
Habari zinaeleza kuwa magari hayo 20, yatawasili na manowari kubwa ya Marekani ambayo inategemea kuwasili nchini wakati wowote kupitia Bahari ya Hindi.
Inaelezwa kuwa kazi nyingine ya manowari hiyo ni kudumisha usalama baharini, kuhakikisha watu wenye lengo la kufanya uvamizi hawafanikiwi kwa njia ya majini katika kipindi hiki cha siku chache kabla ya ujio wa Obama na hata pale akiwepo.

HOTELI ZA NYOTA TANO ZAJAA
Uchunguzi wa Risasi Mchanganyiko  umebaini kuwa ujio wa Obama umekuwa na neema kwa hoteli zenye hadhi ya nyota tano ambazo karibu zote zimekodiwa jumla.
Hoteli hizo zimechukuliwa na Marekani kwa ajili ya watu watakaombatana na Obama ikiwemo wahudumu pamoja na walinzi mbalimbali.
Inaelezwa, baadhi ya hoteli kuna wateja walihamishwa wiki mbili kabla ili kupisha wageni kutoka Marekani ambao wamekuwa wakiwasili nchini kwa mafungu.

WENYE MAGARI MAPYA WAULA
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa wamiliki wa magari mapya yenye nafasi, hususan Toyota Noah, kwao ni neema ya aina yake.
Risasi Mchanganyiko limebaini kuwa wenye magari hayo hutakiwa kuripoti Ubalozi wa Marekani nchini kisha vyombo vyao hupimwa kuona uzima wake.
Habari zinasema, kila mwenye gari ambalo litafuzu vipimo, atalipwa shilingi 200,000 kwa siku katika kipindi chote litakapotumika katika ziara hiyo ya Obama.

BUSH NAYE ANAKUJA
Katika hatua nyingine, Bush ambaye ni Rais wa 43 wa Marekani, atawasili nchini hivi karibuni.
Hii ina maana kuwa kipindi ambacho Obama atakuwepo nchini, Bush naye atakuwepo ndani ya Tanzania.
Bush yeye anakuja kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa wake za marais mbalimbali duniani ambapo imeelezwa kuwa mke wa Obama, Michelle, naye atahudhuria.

 KARIBU OBAMA
Ujio wa Obama ni fahari ya Tanzania kwamba nchi yetu ni salama na inavutia ndiyo maana hata kiongozi huyo wa taifa kubwa kabisa duniani, ameweza kushawishika kuja.
Karibu sana Tanzania Rais Obama. MHARIRI.

TIGO SABASABA BASH INAKULETEA USIKU WA MATUMAINI 2013

dimanche 23 juin 2013

WHERE IS THE MOUSE??

MUUZA SAMAKI NA MTEJA

Mteja; Samaki bei gani?

Muuzaji; 2500.

Mteja; Mwisho?

Muuzaji; Mkiani.

Mteja; Mbona samaki mwenyewe kalegea?

Muuzaji; Labda alikua shoga baharini.

JANET JACKSON ABADILI DINI NA KUWA MUISLAM SAFI-MZIKI NA FILAMU SASA BASI




JANET JACKSON ABADILI DINI NA KUWA MUISLAM SAFI-MZIKI NA FILAMU SASA BASI

Singer Janet Jackson had a widely celebrated wedding to billionaire Wissam Al Mana just a few months ago.  You might have heard that the wedding cost millions of dollars, and since that time, Janet hasn’t done any acting or released any music.

It has since been reported that Janet has moved to the Middle East and converted to Islam.  Surprisingly, she also has disavowed music and left the industry entirely.  Janet says that part of the reason she wants to leave music is so that she and her husband can live a private life away from the media.

Al Mana made his fortune through the Al Mana Retail group, which is owned and controlled by his family.

This is Janet Jackson’s third marriage and her last major media appearance was in a Tyler Perry film, “Why Did I Get Married?”

Janet is now 47-years old and still looking great.  She got her big break in 1982 after releasing the album control.   We will always love Janet, whether she lives in the US, the middle east or anywhere else.

TOA MAONI YAKO HAPA

samedi 22 juin 2013

vendredi 21 juin 2013

HII NDIO BUSTANI YA MAPENZI YA MULIRO ILIYOPO NCHINI KENYA








Hii ni Bustani iliyopata umaarufu sana huko kwa majirani zetu ...hapo watu bila aibu wanatumia hiyo bustani kama Gesti ....Picha hizi jamaa walitega kamera na kuchukua picha na video za watu tofauti katika nyakati tofauti...

Diamond Aachia video ya ukimwona

Diamond Aachia video ya ukimwona:
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ ameisambaza video ya ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Ukimwona'

JINSI WANAWAKE WANAVYOSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA WANAUME ZAO

1: KAULI
Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo litampelekea kupotea nguvu za kiume taratibu.

Msaada unaohitajika kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwambia hawezi, bali ni kumtia moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwaambia maneno kama haya: “Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”


2 : UJUZI

Wanawake wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa. Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili humfanya mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.

Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni watundu mno kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume ajione kama mgeni wa mchezo huo.

Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Inashauriwa kwamba, mwanamke anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo, asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama mwanafunzi, asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko vya juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi huwaogopesha wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.

3:USAFI
Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi na mwili ni muhimu sana katika mapenzi.

4:GUBU
Jambo lingine linaloweza kumsababishia mwanaume upungufu wa nguvu za kiume ni gubu au karaha za maneno ya uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Uchokonozi wa mambo, ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa na staha ni mambo yanayosababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Mwanamke anapokuwa mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na matusi huweza kumfanya mume amchukie na kutopenda kushiriki naye tendo. Uchunguzi unaonesha kwamba wanawake walioolewa wenye tabia hii, huwafanya waume zao wawe na msisimko wa kimapenzi kwa wanawake wa nje kuliko wake zao hao.

5:USALITI
Tabia ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo kingine cha mwanaume kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Mwanaume anapoona, kuhisi au kubaini kuwa anasalitiwa, huumia sana moyoni, maumivu ambayo hatimaye humfanya muhusika kuwa na mawazo mengi ambayo humuondolea hamu ya tendo.


Dokta Bianca P. Acevedo kutoka Chuo Kikuu cha California

vendredi 14 juin 2013

Tacle assassin

JE BINTI WA KIRUNDI ANAWEZA VAA NA KUTEMBEA MTAANI KAMA HUYU?


Hii inatokea huko kwa Mswati Je Msichana wa Kirundi Unaweza Vaa na Kutembea Mtaani Kama huyu?
TOA MAONI YAKO HAPA

Stamina Aandaa WAZO LA LEO [REMIX]... Je MwanaFA Atakuwemo??



Rapper kutoka MORO TOWN, Stamina Kabwela seem to be busy now kutengeneza remix ya ngoma kali inayojulikana kama WAZO LA LEO...
Stamina ameonekana kufanya hivyo hasa baada ya original version ya ngoma hiyo kufanya vizuri sana akiwa ameshirikisha rapper kutoka Rock City [MWANZA] Fid Q...
Stamina ameshawishika kufanya hivi as in fans pia kutaka kuona wakali wengine wa hip-hop ambao wanafanya kama yeye wanawezaje kuonesha umahiri kwenye mdundo mkali huo wa Producer P-Funk Majani [BONGO RECORDS].
Earlier today, rapper Stamina alionekana kumu-approach rapper mwingine mkali kutoka TANGA, Hamis Mwinjuma famously known as MwanaFA na kumuhitaji kushiriki katika remix hiyo...
This is how it went down... Stamina (@StaminaKabwela on twitter) alianza,"FA fresh bro nafanya rmx ya wazo la leo nakuhitaji braza kwa uwepo wako wa mistari 8 tu kama inawezekena"... Stamina wouldnt ask for more kutoka kwa braza MwanaFA but mistari 8... #HipHop
MwanaFA (@MwanaFA on twitter) replied, "Tuongee kwenye simu bro..."
Stamina amekuwa ni msanii mpya kwenye game la hip-hop hapa Bongo akifanya vizuri kwa takribani tracks 4 au 5 sasa... He's making WAZO LA LEO remix... And MwanaFA can surely fit on this one...

Swali : Je MwanaFA atakuwemo kwenye remix hiyo??
Naamini mimi na wewe tunaruhusiwa kusubiria hii... Stay Tuned !!
Source: GongaMx

TOA MAONI YAKO HAPA

Langa kuzikwa Jumatatu kwenye makaburi ya Kinondoni

Langa kuzikwa Jumatatu kwenye makaburi ya Kinondoni
33c2e-wak

AIBU:WANAFUNZI WA CHUO MTWARA WAFANYA PARTY YA KIF...

AIBU:WANAFUNZI WA CHUO MTWARA WAFANYA PARTY YA KIF...:   Ndani ya pub hiyo, madenti hao  walianza  kwa  staili  ya  kupiga  pombe  kabla  ya  michezo ya  kifusika  kuanza... Pombe  ...





 Ndani ya pub hiyo, madenti hao  walianza  kwa  staili  ya  kupiga  pombe  kabla  ya  michezo ya  kifusika  kuanza...

Pombe  ilipowakolea, madenti  hao  waligawana, kila  mtu  mtu  na  wake  na  kuanza  kubadilishana  mate  na  michezo  mingine  ya  michafu...
Hali  hiyo  ilizua taflani  kubwa  kwa  wananchi waliokuwa  eneo  hilo huku  wengine  wakionekana  kutoamini  macho  yao  kwa  vitendo  vilivyokuwa  vikitendwa  na  madenti  hao..

dimanche 9 juin 2013

Hii Ndio list ya Walio pata Tuzo Kilimanjaro Music Awards 2013


 Host wa tuzo hizo mwaka huu alikuwa ni Zembwele na TJ.

Hii ni list nzima ya tuzo hizo.

Wimbo bora wa mwaka
Dear God – Kala Jeremiah

Msanii bora wa Kiume
Diamond

Msanii bora wa kike
Lady Jaydee

Msanii bora wa kike Taarab
Isha Mashauzi

Msanii bora wa kiume Taarab
Mzee Yusuf

Msanii bora wa kiume Bongo Flava
Diamond

Msanii bora wa kike Bongo Flava
Recho

Msanii bora wa Hip Hop
Kala Jeremiah

Msanii bora wa kiume Bendi
Chalz Baba

Msanii bora wa kike Bendi
Luiza Mbutu

Msanii bora anayechipukia
Ally Nipishe

Video bora ya mwaka
Baadaye – Ommy Dimpoz

Mtunzi bora wa mashairi Taarab
Mzee Yusuf

Mtunzi bora wa mashairi Bongo Flava
Ben Pol

Mtunzi bora wa mashairi hip hop
Kala Jeremiah

Mtunzi bora wa mashairi Bendi
Chalz Baba

Mtayarishaji bora wa mashairi muziki wa kizazi kipya
Man Walter

Mtayarishaji wa wimbo wa mwaka – Taarab
Enrico

Mtayarishaji wa wimbo mwaka – Bendi
Amoroso

Mtayarishaji chipukizi wa mwaka
Mesen Selekta

Rapper bora wa bendi
Fagasoni

Wimbo bora wenye vionjo vya asili
Chocheeni Kuni – Mrisho Mpoto ft Ditto

Wimbo bora wa bendi
Risasi Kidole – Mashujaa Band

Wimbo bora wa Reggae
Kilimanjaro – Warriors from The East

Wimbo bora wa Afrika Mashariki
Valu Valu – Jose Chameleone

Wimbo bora wa Bongo Pop
Me an You – Ommy Dimpoz ft Vanessa Mdee

Wimbo bora wa kushirikiana/Kushirikishwa
Me and You – Ommy Dimpoz ft Vanessa Mdee




Wimbo bora wa Hip Hop
Nasema Nao – Nay wa Mitego

Wimbo bora wa rnb
Kuwa na Subira – Rama Dee ft. Mapacha

Wimbo bora wa ragga/ dancehall
Predator – Dabo

Wimbo bora wa Taarab
Mjini Chuo Kikuu – Khadija Kopa

Wimbo bora wa zouk rhumba
Ni wewe – Amini

Bendi bora ya mwaka
Mashujaa Band

Kikundi bora cha Taarab
Jahazi Modern Taarab

Kikundi bora cha muziki wa Kizazi kipya
Jambo Squad

Hall of Fame – Institution
Kilimanjaro Band wana Njenje

Hall of Fame – Individual
Salum Abdallah

Usiku wa tuzo za KTMA ulipambwa na burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiwemo Linah, Amini, Richie Mavoko, Mataluma, Hussein Jumbe, Zahir Zorro, Patricia Hillary na Barnaba. Wengine ni Snura, Godzilla, Mabeste, Madee na Afande Sele.

lundi 3 juin 2013

NEYMAR ATUA RASMI BARCELONA





Klabu ya Barcelona imemtambulisha rasmi mshambuliaji wake mpya, Neymar da Silva Santos Júnior 'Neymar' klabuni hapo kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kuanza kuitumikia timu hiyo. Pichani juu ni baadhi ya taswira za mchezaji huyo akiwasili klabuni hapo.

lolilo ft Diamond nkarira

http://www.hulkshare.com/9e8mi7ui7y4g

samedi 1 juin 2013

KIFO CHA MANGWEA NI SUMU!

Stori:Sifael Paul
KIFO cha msanii wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangwea a.k.a Ngwea kilichotokea Jumanne wiki hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini ‘Sauzi’, kinaendelea kuibua mapya ambapo sasa sumu imetajwa kuhusika, Risasi Jumamosi linafungua kila kitu.
Hospitali aliyopelekwa
Akizungumza na paparazi wetu juzi kwa njia ya simu moja kwa moja kutokea nchini humo, Mtanzania mmoja (jina tunalo) alisema muda huo yeye alikuwa nje ya Hospitali ya St. Helen Joseph ambako mwili wa marehemu ulikuwa umehifadhiwa kwenye Mochwari ya Hillbrow.
M2 The P akiwa amelazwa Hospitali
Mbongo huyo alisema alifanikiwa kuutazama mwili wa marehemu Ngwea ambapo ulionesha kuwa wakati wa kukata roho damu nyingi zilimtoka kupitia puani na mdomoni kiasi cha kuwashangaza wauguzi.
Mwili wa Marehemu
NI SUMU
Alisema muuguzi mmoja aliyekuwa akimtibu mshirika wa marehemu, Mgaza Pembe a.k.a M2 The P aliyenusurika, alimwambia wawili hao walionekana kuingiwa na kitu cha hatari na kibaya sana mwilini jambo lililowashtua hata madaktari wenyewe.
Mama mzazi wa mangwea akiwa kwenye huzuni
Alisema muuguzi huyo alimweleza kuwa kitu walichokula au kulishwa kiliwadhuru sana ndani ya miili yao na kusababisha mishipa ya damu kwa Mangwea kupasuka hovyo kwa kuwa moyo ulizidiwa na presha ya msukumo wa damu.
Mtanzania huyo alidai kuwa hata kama kweli wawili hao walichanganya vileo kama watu wanavyodai, basi ule mchanganyiko ndiyo uliotengeneza sumu mwilini akisisitiza kuwa hilo halina shaka kwa mujibu wa muuguzi huyo.
Eneo atakalozikwa
“Unajua kuna watu wanapenda kuchanganya pombe kali kwa hiyo kuna wanaodai wawili hao walichanganya ‘unga’, bangi na pombe kali. Mchanganyiko huo tu wenyewe ni sumu tosha mwilini kwa binadamu yeyote yule.
“Wataalam wanajua, ukichanganya pombe kali unapata upungufu wa oksijeni katika damu hivyo unaupa moyo kazi ya ziada ya ‘kupampu’ damu kwa kuwa presha inakuwa kubwa. Kwa hiyo kinachotokea ni kupasuka kwa mishipa mikubwa ya damu, ndiyo maana damu zilitoka puani na kinywani kwa wingi.
“Kwa kuchanganya vileo hivyo unatengeneza sumu ambayo husababisha shambulio kubwa la damu na mfumo wa upumuaji kushindwa kufanya kazi.
“Sasa usipowahishwa hospitali ili kuchomwa sindano ya limao, kifo kinakuwa njenje.
“Kwa vyovyote walikula au walilishwa sumu, daktari anasema mwili wa Ngwea umeharibika sana kwa ndani.
 “Kile siyo kipigo, hakuna jeraha lolote la kupigwa, ile ni sumu,” kilidai chanzo hicho cha kuaminika.

SAA CHACHE KABLA YA KIFO
Habari za kina kutoka kwa mmoja wa watu waliokuwa nao kabla ya kukutwa na tukio hilo zilieleza kwamba kabla ya kwenda kulala, Ngwea na mwenzake, walikutana na baadhi ya Watanzania waishio Sauzi na kupiga stori kwenye baa moja huku wakitaja majina ya wasanii wa Bongo Fleva waliotangulia mbele ya haki.
Ilidaiwa kuwa kila jina la msanii marehemu lilipotajwa Ngwea alikuwa akitamka ‘OMG’ (Ooh! My God) yaani Ooh! Mungu Wangu, bila kujua kitakachomkuta baadaye.

MADAI MENGINE, MAISHA YA SAUZI
Kuna madai mengine kwamba baadhi ya Wabongo waishio Sauzi huwa wana maisha ya kutegana hasa wakijua Mtanzania mwenzao kaenda kule akiwa na ‘mkwanja’ mrefu.
“Tatizo lingine ni kwamba kama walifanyiziwa na mtu huo uwezekano ni mkubwa sana kwani huku jamaa wakikushtukia tu kuwa una mkwanja, kwanza wanakuwa karibu sana na wewe ‘then’ ukikaa vibaya lazima wakutoe uhai.
“Inawezekana akina Ngwea walifanyiziwa kwa kulishwa sumu kwa sababu walikuwa wameshapiga mkwanja tayari kwa kurejea Bongo,” alisema Mbongo huyo.

MCHUNGAJI ALIKIONA KIFO CHAKE MAPEMA!
Mwezi Machi mwaka huu, kupitia gazeti tumbo moja na hili, Ijumaa la Machi 22-28, 2013 liliandika ukurasa wa mbele habari yenye kichwa; ‘MASTAA WAWILI KUFA MWAKA HUU’ ambapo mchungaji maarufu jijini Dar alisema mwaka 2013  ameona katika maono yake vifo vya wasanii wawili wa Bongo.
Katika habari hiyo, mchungaji huyo alitahadharisha mapema kuwa wasanii wamrudie Mungu kwani upepo siyo mzuri kwao.
Mchungaji huyo alieleza: “Mwaka huu ulipoanza, Januari 2, Sajuki (Juma Kilowoko) aliaga dunia katika Hospitali ya Muhimbili alikolazwa lakini nimepewa maono na Mungu kwamba wasanii wengine wawili watakufa mwaka huu.
“Katika hayo maono niliona wasanii wenyewe, mmoja wa kike, mwingine wa kiume. Wa kike ni msanii wa filamu, wa kiume anaimba hizi nyimbo za kisasa za Bongo Fleva.
“Huyo wa Bongo Fleva siyo mkongwe sana kama wale waanzilishi wa fani hiyo lakini anajulikana sana na mashabiki wengi. Nyimbo zake zinajulikana pia.
“Huyu wa kike yeye ni mkongwe kidogo, halafu ni mweusi, zamani aliwahi kuwika sana lakini kwa siku za hivi karibuni amepoapoa.”

MANENO YAKE YALIJAA UTABIRI
Watu wa karibu waliokuwa wakichati na Ngwea kupitia mitandao ya kijamii walisema siku za mwisho wa uhai wake, marehemu alipenda kutumia maneno yenye kumtaja Mungu, Yesu au viashiria vingine vinavyofanana  na hivyo.

TURUDI KWENYE TUKIO
Habari zilieleza kuwa baada ya majibu ya kilichomuua Ngwea kujulikana, mwili wa staa huyo utaagwa kesho jijini Dar ambapo msiba upo kwa kaka yake Mbezi Beach na baadaye mwili utasafirishwa kwenda mkoani Morogoro eneo la Kihonda, nyumbani kwao.

NGWEA HAPA, BABA’AKE PALE
Habari kutoka msibani Morogoro zimeeleza kwamba marahemu Ngwea atazikwa jirani kabisa na kaburi alilozikwa marehemu baba yake, mzee Kenneth Mangwea. Huo ni ushauri wa familia yake.

HALI YA M2 THE P
Kwa upande wake, M2 The P, hadi gazeti linakwenda mitamboni alikuwa akiendelea na matibabu huko Sauzi huku hali yake ikisemekana inaendelea kuimarika.
Ngwea alizaliwa Novemba 16, 1982 huko mkoani Mbeya (asili yake ni Mkoa wa Ruvuma) akiwa mtoto wa mwisho katika familia yao. Hajaacha mke wala mtoto.

bêtisier foot