Alibaba

jeudi 22 septembre 2016

Tiwa Savage akava jarida la Vibe

Diva wa muziki wa Nigeria, Tiwa Savage amekava jarida la Vibe la Marekani kwenye toleo litakalotoka mwisho wa mwezi huu.

Muimbaji huyo amefunguka mambo mengi kwenye jarida hilo ikiwemo mwanzo alipoanzia mpaka kuingia kwenye muziki, maisha yake na mambo mengine mengi.

“I played trombone. Don’t ask me if I still play [laughs], but I literally picked it up because I had a crush on a boy in high school. He used to hang around with the cool kids, the musicians and dancers. Here I was: this kid fresh from Nigeria, strong accent, my mom shaved my hair off,”

amesema Tiwa kwenye jarida hilo.

“I tried to get his attention. I went to this music teacher and said that I really wanted to do music. He looked to the corner of the room and said the trombone was the only instrument left. I picked it up, but eventually got bullied for it because it was always getting in the way on the bus.”

“That was having the opposite effect of what I wanted because this guy’s now laughing at me instead of falling in love with me. So, I gave up and joined the choir.”

Hii ni mara ya pili kwa msanii huyo kutokea kwenye majarida tofauti ndani ya mwezi mmoja, alitokea kwenye jarida la Elle la Afrika Kusini mwezi uliopita.

Tuzo za MTV MAMA 2016 wasani watajwa, nao ni…

Orodha ya wasanii watakaowania tuzo za MTV MAMA 2016, Jumamosi ya Oktoba 22 kwenye ukumbi wa Ticketpro Dome, Afrika Kusini imetoka – kuna vipengele tisa. Tanzania inawakilishwa na Alikiba, Diamond na Navy Kenzo.

Hii ni orodha kamili ya wasanii waliochaguliwa kuwania tuzo hizo

Best Live Act
Stonebwoy (Ghana)
Cassper Nyovest (South Africa)
Mafikizolo (South Africa)
Mr Flavour (Nigeria)
Eddy Kenzo (Uganda)

Best POP/ ALtenative
Tresor – Never let Me Go
Shekinah & Kyle Deutsch – Back to the Beach
Timo ODV – Find My Way
LCVL ft Sketchy Bongo – Cold Shoulder
Desmond & The Tutus – Pretoria Girls

Personality of the Year
Caster Semenya
Linda Ikeji
Pearl Thus
Wizkid
Pierre Emerick

Best Group
Toofan (Togo)
Micasa (South Africa)
Navy Kenzo (Tanzania)
R2Bees (Ghana)
Sauti Sol (Kenya)

Best Male
Black Coffee (South Africa)
Diamond Platnumz (Tanzania)
AKA (South Africa)
Patoranking (Nigeria)
Wizkid (Nigeria)

Best Lusophone
NGA
Nelson Freitas
C4 Pedro
Lizha James
Preto Show

Best International Act
Beyonce
Drake
Adele
Future
Rihanna

Best Collaboration
AKA ft Yanga, Burna Boy, Khuli Chana – Baddest
Dj Maphorisa, ft Wizkid, Dj Buckz – Soweto Baby
Nasty C ft Davido, Cassper Nyovest – Juice Back (Remix)
Sauti Sol ft Alikiba – Unconditionally Bae
Patoranking ft Sarkodie – No Kissing

Best Hip Hop
Emtee (South Africa)
Ricky Rick (South Africa)
YCEE (Nigeria)
Olamide (Nigeria)
Kiff No Beat (Ivory Coast)

Wakala wa Yaya Toure akataa masharti ya Guardiola

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amejipata katika vita vya maneno na wakala wa kiungo wa kati Yaya Toure baada ya kukosa kumteua kiungo huyo katika kikosi cha wachezaji 25 watakaoshiriki katika mechi za klabu bigwa barani Ulaya katika hatua ya makundi.

Guardiola amesema hatamteua mchezaji huyo hadi pale wakala wake Dimitry Seluk, atakapoomba msamaha kwa matamshi aliyotamka kwa vyombo vya habari.

Lakini ajenti huyo amesema katu hatafanya hivyo na badala yake akasisitiza kwamba meneja huyo ndiye afaaye kuomba radhi.

''Kwa nini ni muombe msamaha Guardiola? Sijui maneno ninayostahili kutamka kuomba radhi, kwa sababu sijafanya kitu chochote. Iwapo nitajihisi kuomba radhi, basi nitaomba radhi hiyo, lakini sihisi kufanya hivyo. Kile Guardiola anachokitaka hakitawezekana,'' alisema Seluk kwenye runinga ya Sky Sport News.

Amesema meneja huyo amewakosea watu wengi akigusia mtangulizi wake Manuel Pellegrini na kisha kipa nambari moja wa Manchester City Joe Hart ambaye alilazimika kuondoka klabu hiyo majira ya joto baada ya kuachwa nje ya mipango ya Guardiola.

"Ni lazima awaombe radhi Yaya na Hart na Pellegrini. Guardiola anashinda mechi kadha na kuanza kufikiria kwamba yeye ni mfalme."

Seluk amesema mteja wake, Toure ,33, ameshiriki katika mechi moja kati ya mechi nane walizozicheza Manchester City msimu huu.

Guardiola amesema iwapo Seluk atamuomba msamaha yeye, klabu hiyo na wachezaji wa timu hiyo hapo ndio Yaya atakuwa na nafasi sawa ya kushiriki katika michezo yote.

''Sitakubali kama kocha kila ajenti, kwenda kwa vyombo vya habari kuwasilisha malalamiko yao iwapo mchezaji wake hajashirikishwa kweye kikosi," Guardiola ameongezea.
Guardiol alikuwa kocha wmkuu Barcelona Toure alipouzwa kwa Manchester City mwaka 2010.