Google tag

mardi 25 octobre 2016

Wenger: Tuna fursa nzuri ya kushinda ligi

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ana fursa nzuri ya kushinda ligi ya Uingereza msimu huu kwa mara ya kwanza tangu washinde taji hilo bila kushindwa mwaka 2004.

Akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa klabu hiyo,Wenger mwenye umri wa miaka 67,alisema kuwa mshindi wa taji la ligi kuu atakuwa na kati ya pointi 82 na 86 mwaka huu.

Alisema: Hii leo tuko katika nafasi nzuri zaidi ya kuwania taji la ligi ya Uingereza ikilinganishwa na miaka mitano au sita iliopita.

Ninaamini tuna timu nzuri katika ligi yenye ushindani mkubwa.
Arsenal ni wa pili katika jedwali la ligi,ikiwa ni mojwapo ya timu tatu zenye pointi 20 na wako katika nafasi ya pili kutokana na tofauti ya mabao.

Wenger anasema kuwa anafikiri kwamba anahitaji pointi 62 kutoka kwa mechi 29 zilizosalia kushinda taji .

Leicester ndio mabingwa wa taji hilo msimu uliopita.
''Baada ya mechi 9 ,tuna pointi 20,ikimaanisha kwamba ubingwa huo utaamuliwa na kati ya pointi 82 na 86'',alisema.

Aliyekuwa beki wa Brazil Carlos Alberto afariki

Aliyekuwa mchezaji mashuhuri wa timu ya Brazil Carlos Alberto ,ambaye alikuwa nahodha wa kikosi kilichoshinda kombe la dunia mwaka 1970 amefariki akiwa na umri wa mika 72.

Alifunga mojawapo ya mabao mazuri zaidi duniani katika historia ya kombe la dunia katika mechi ya fainali dhidi ya Italy mwaka 1970,baada ya kuwachenga mabeki na kufunga kupitia mkwaju mkali.

Beki wa kulia Alberto alichezeshwa mara 53 na Brazil na kushinda mataji ya nyumbani dhidi ya Fluminense na Santos ambapo alishiriki mara 400.

Alifariki mjini Rio de Janeiro kufuatia mshtuko wa moyo.

Zamalek yasema "uchawi" uliwafanya kushindwa

Mwenyekiti wa Zamalek Mortada Mansour amelaumu "uchawi na bahati mbaya" kwa kushindwa kwa timu yake mikononi mwa timu ya Afrika Kusini ya Mamelodi Sundowns katika fainali ya ligi kuu barani Afrika.

"Kulikuwa na nafasi nyingi kwetu sisi katika mechi zote, lakini mpira ulikataa kutingiza nyavu" Mansour aliongeza, baada ya kushindwa mabao 3-1 kwa jumla ya mabao.
Pia aliunga mkono kwa kocha Moamen Soliman kusalia katika nafasi yake licha ya kupoteza.

"Tuna wakufunzi wazuri na sitawafuta kazi," amesema Mansour, mbaye aliwatumia wakufunzi sita mwaka huu.

"Kocha Moamen atasalia kama mkufunzi mkuu wa Zamalek, hadi mwisho wa msimu huu."

Ballon d'or 2016 wanao baki

Mshambuliaji wa timu ya Wales Gareth Bale na mwenzake wa Real Madrid Cristiano Ronaldo wameorodheshwa kuwania taji la mchezaji bora duniani mwaka 2016 Ballon d'Or.

Wachezaji wa Manchester City Sergio Aguerro na Kevin De Bruyne, pamoja na wachezaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann pia wako katika orodha hiyo.

Gazeti la soka la Ufaransa limebaini orodha ya wachezaji 30 katika makundi ya wachezaji watano kila baada ya saa mbili siku yote ya Jumatatu.

Tuzo hiyo hutolewa na Ufaransa kila mwaka tangu mwaka 1956, lakini kwa kipindi cha miaka sita iliopita tuzo hiyo ilibadilika na kuwa Fifa Ballon d'Or kwa ushirikiano na shirikisho la soka duniani Fifa.
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi alishinda tuzo hiyo mwaka uliopita kwa mara ya tano .

*Wachezaji waliorodheshwa ni:

Sergio Aguero (Manchester City),
Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund),
Gareth Bale (Real Madrid),
Gianluigi Buffon (Juventus),
Cristiano Ronaldo (Real Madrid),
Kevin de Bruyne (Manchester City),
Paulo Dybala (Juventus),
Diego Godin (Atletico Madrid),
Antoine Griezmann (Atletico Madrid),
Gonzalo Higuain (Juventus).