Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa msiu wa klabu hiyo kupitia kipengele cha Sir Matt Busby Mchezaji Bora wa Mwaka kutokana na uchezaji wake katika klabu ya Manchester United msimu wa 2021/22.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alirejea Old Trafford msimu uliopita wa joto na kufanikiwa kufunga mabao 24 katika mashindano yote.
Ingawa ilikuwa msimu mgumu kwa klabu hiyo ikishika nafasi ya sita na kufika tu hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa, Ronaldo aliwahi kuwa miongoni mwa mastaa wachache waliokuwa na msimu bora msimu huu.
Katika msimu huu Ronaldo alishinda tuzo hiyo mara tatu - 2003/04, 2006/07 na 2007/08 - lakini ameshinda kura wakati huu na kufikisha tuzo zake nne za Mchezaji Bora wa Mwaka wa Sir Matt Busby. kama ilivyo kwa ManUtd.com.