Stori: Shakoor Jongo na Musa Mateja
WAKATI zilipendwa wake Nasibu Abdul ‘Diamond’ akifuturisha kila
kukicha, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ametupiwa madongo mazito
akiambiwa amejinajisi Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kufuatia picha zake
zisizopendeza kipindi cha mfungo kutumbukizwa mtandaoni, Ijumaa Wikienda
linakupa habari kamili.
Moja ya picha alizotupia Wema Sepetu.
Julai 19, mwaka huu (Chungu cha Kumi)
picha za Wema ambaye ni staa wa filamu za Bongo na Miss Tanzania mwaka
2006/07 ziliingizwwa mtandaoni akiwa katika mapozi mbalimbali yenye
‘kuuchefua’ mwezi kama mtu atakumbana nazo.
Picha moja ilimuonesha mrembo huyo akiwa ‘klozidi’ na meneja wake, Martin Kadinda. Wanaonekana wamekumbatiana.
Picha nyingine inamuonesha Wema akipiga mbizi kwenye swimming pool moja ambayo haikufafanuliwa ni wapi nchini Tanzania.
Mbali na picha hizo mbili, nyingine ilimuonesha mlimbwende huyo akiwa
katika gauni jepesi kiasi cha kuweza kuonesha ‘nido’ zake.
Diamond (wa pili kulia) akifuturu na watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa Bongo.
WACHANGIAJI SASA
“Dah! Nimemshangaa
sana Wema, amekubali vipi kuweka picha zake kwenye neti katika kipindi
hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, maana hazistahili kabisa,” alisema
mmoja wa wasomaji wetu ambaye alibahatika kuziona picha hizo.
Msomaji huyo aliendelea kusema kwamba kwa uzoefu wake kipindi hiki cha
mfungo ‘blogi’ nyingi (akimaanisha mitandao) zinaweka picha za watu
wakifuturu, wengine wakifuturisha, alimshangaa Wema ni Muislamu safi
lakini kumbe si mfuataji wa maadili ya imani.
“Wema amejinajisi tu
kwa Mwezi wa Ramadhani, picha zilizoko kwenye mtandao siyo kabisa,
ikiwezekana azitoe ataziweka tena baada ya mfungo kwisha,” alimalizia
kusema mtu huyo.
Wachangiaji wengine hawakuwa mbali sana na wa
kwanza, nao walionesha kukerwa kwao na jinsi picha hizo zilivyotupiwa
mtandaoni katika kipindi hiki cha toba na kusema funga ya Wema ni bure.
Diamond katika vazi la kanzu.
AWALI YA YOTE
Kabla ya kumsaka Wema,
Ijumaa Wikienda lilijiridhisha kwamba, mtandao uliotumika kutupiwa picha
hizo zilizowakera baadhi ya watu si wa Wema, bali ni wa meneja wake,
Martin Kadinda.
WIKIENDA LAANZA NA WEMA
Licha ya
kutambua hilo, Jumamosi iliyopita, Ijumaa Wikienda lilianza kwa kumsaka
Wema kwa njia ya simu ya kiganjani ili kumuuliza kama ana amani moyoni
kufuatia picha zake zilizotafsiriwa kuwa ni za kuinajisi swaumu yake
kutumbukizwa mtandaoni, lakini simu yake haikupatikana hewani.
Wema katika vazi la hijabu.
KADINDA APATIKANA, HEBU MSIKIE
Baada ya kumkosa Wema ndipo Ijumaa
Wikienda lilipomsaka Kadinda ili kuisikia kauli yake hasa ikizingatiwa
kuwa, mtandao uliotumika ni wa kwake.
“Hivi ngoja nikuulize, mtu
akifunga haruhusiwi kuingiza, kuangalia picha mtandaoni au haruhusiwi
kuogelea? Isitoshe picha hizo zilipigwa kabla ya Mwezi wa Ramadhani
ilikuwa siku ya vunja jungu, siku moja kabla ya kuanza kwa Ramadhani,”
alisema Kadinda.
Wikienda: Lakini hata kama ilikuwa vunja jungu, sasa ni kwa nini umeziweka picha zile kipindi hiki?
Kadinda: Kwani kuna tatizo?
Wikienda: Wee huoni kama umeinajisi funga ya mwenzako katika mwezi huu?
Kadinda: Mimi sijaona tatizo.
Wikienda: Kwa nini usingesubiri mfungo ukaisha ndipo utupie zile picha?
Maana kwa sasa wengi wanatupia picha za kufuturu au kufuturisha.
Kadinda: Tatizo liko wapi kwani?
Ijumaa Wikienda liliamini Kadinda hakuwa tayari kukiri, likaachana naye.
MASTAA WAGOMBEA FUTARI KWA DIAMOND
Wakati Wema yakimkuta hayo, naye Diamond, Ijumaa iliyopita aliendelea
na kufanya suna kwa kufuturisha watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa
Bongo.
Wengine walioalikwa kufuturu ni watoto yatima kutoka vituo vinne vya jijini Dar.
Diamond alilifanya zoezi hilo nyumbani kwake, Sinza-Mori, Dar ambako anaishi na mama yake mzazi, Sanura Kasim ‘Sandra’.
Baadhi ya mastaa waliohudhuria mwaliko huo wa futari walionekana
kugombea kutokana na watu kuwa wengi huku futari ikiwa kidogo kuliko
wafungaji.
“Watu ni wengi lakini kwa mtazamo wangu naona kama futari
yenyewe ni ndogo,” alisema memba wa Tip Top Connection, Hamad Ally
‘Madee’.
DIAMOND AGAWA ‘WEKUNDU’
Baada ya kumaliza kufuturu
na watu kutoa shukurani zao kwa Diamond huku wengine wakimpongeza kwa
hatua hiyo, ghafla msanii huyo aligeuka pedeshee kwa kutoa noti za
shilingi elfu kumikumi ‘wekundu’ kwa kila mtoto yatima aliyehudhuria
futari hiyo.
“Unajua kwenye hii futari ukiacha marafiki, ndugu na
jamaa, kuna watoto yatima kutoka vituo vinne na kila kituo wamekuja
watoto kumi na ndiyo hao peke yao nimewapa fedha kama sadaka yangu,”
alisema Diamond alipoulizwa na waandishi mara baada ya kumaliza zoezi
hilo.
APONDWA, ADAIWA SI MSAFI SANA
Licha ya futari hiyo ya
kuwepo yatima, lakini wapo watu waliosema msanii huyo si msafi sana kwa
vile siku kadhaa nyuma, alipiga picha akifuturu na demu wake (hawara),
Peniel Mungilwa ‘Penny’ jambo walilolisema halina baraka Kiislamu kwa
kuwa si mke wake wa ndoa.
APINGWA KUMWAGA PESA HADHARANI
Wakati wengine wakiponda usafi wa msanii huyo kwa kufuturu na kimada,
wapo waliohoji kama Kuran inakubaliana mtu kutoa sadaka ya fedha kwa
wasiojiweza huku wengine wakishuhudia (kama alivyofanya kwa yatima).
“Uislamu hausemi hivi. Uislamu unasema hivi, ukiwa unatoa sadaka kwa
yatima au wasiojiweza, mtu mwingine asione ndiyo baraka zako zipo hapo,”
alisikika akisema mwalikwa mmoja.