Stori: Shakoor Jongo na Imelda Mtema HUKU
mchumba’ke, Penniel Mungilwa ‘Penny’ akifungasha virago kurejea kwao,
mzee mzima Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametangaza kumuoa Miss
Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’(kushoto) na Penniel Mungilwa ‘Penny’ wakiongea jambo enzi za mapenzi yao.
Ishu hiyo ilijiri ndani ya Viwanja vya
Leaders Club, Kinondoni jijini Dar ambapo mkali huyo wa Bongo Fleva
alikuwa akikamua kwenye sherehe ya Krismasi aliyoiandaa mwenyewe.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ baada ya kupanda jukwaani katika viwanja vya leaders.
TANGAZO LA AWALI Awali kabla ya kufikia eneo la kutangaza kuoana, Diamond aliweka wazi jukwaani kwamba yeye na Wema wamerudiana.
Diamond Platnumz akiongea jambo baada ya Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kupanda jukwaani.
MTIRIRIKO ULIVYOKUWA
Diamond, akiwa ameshika kipaza sauti alikatisha kuimba na kuwauliza
mashabiki wake, hasa watoto waliohudhuria kwa wingi tamasha hilo, je,
wanataka kumuona shemeji yao?
“Itakuwa si vizuri mkaondoka bila
kumuona shemeji yenu, nikuleteeni mumuone?” aliuliza Diamond. Swali
hilohilo akalirudia tena ambapo lilipokelewa kwa shangwe huku mashabiki
wakilitaja jina la Wema.
Diamond Platnumz na
Wema Isaac Sepetu wakijiachia.
WEMA APANDISHWA JUKWAANI Kufuatia kelele za
mashabiki, Diamond alimuomba Disco Joker (DJ) wake amuwekee Wimbo wa
Ukimwona ambao ulisindikiza ujio wa Wema jukwaani akifuatana na wapambe
wa Diamond.
“DJ acha huo, nipigie Wimbo wa Ukimwona watu wangu wa
nguvu wamwone shemeji yao kwani tangu nilivyokwenda naye China walikuwa
wakisumbuliwa na maneno tofautitofauti kutoka kwenye mitandao ya
kijamii,” alisikika Diamond.
Diamond, akiwa ameshika kipaza sauti akiima Wimbo wa Ukimwona na Wema akiwa amemkumatia.
JUKWAA SASA Hali haikuwa ya kawaida jukwaani
kwani kilichofuata hapo ni Wema kuonesha kwa vitendo mambo yaliyoashiria
kuwa, wawili hao sasa ni mwendo mdundo.
Wema alishuhudiwa
akimzungushia mikono Diamond kwenye kiuno jambo ambalo liliwafanya
baadhi ya mashabiki wa mastaa hao kutoa machozi ya furaha kuona penzi la
wawili hao limerudi upya, wengine walimwambia Diamond amuoe Wema.
“Diamond muoe Wema, mnapendezana sana,” walisikika mashabiki.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’akimuaga Diamond Platnumz kwa kumkumatia.
MAWIFI WADAI KUHARIBIWA SIKU NA KAKA YAO Hata
hivyo, kitendo cha Diamond kumwita Wema jukwaani kilionekana kuharibu
furaha ya sikukuu kwa ndugu zake kwani bila ya kuuma midomo dada zake
staa huyo wakiongozwa na Esma Khan walinuna na kuanza kuondoka.
“Yaani siku yangu imeshaharibika, nilikuja nina furaha sasa imepotea,
tuondokeni ndugu zanguni,” alisema Esma akiwaambia Mwanaisha Abdul
‘Queen Darleen’ na Halima Haroun ‘Kimwana’.
Diamond Platnumz na Penny wakiwa pamoja enzi za mapenzi yao.
MAMA DIAMOND ASHANGAA Kitendo cha ndugu hao
kukasirika hakikupokelewa vizuri na bi mkubwa wao yaani mama Diamond,
Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye aliwajia juu akiwashangaa.
“Wajinga
nini? Sasa walitaka Diamond… (tusi) wao, mtu ameshaamua kupenda
wamwache, mi’ mwenyewe nimeshajifunza, sitaki kuingilia penzi lake,”
alisema mwanamke huyo ambaye mjini anazungukia usafiri aina ya Altezza.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Baada ya shoo hiyo iliyomalizika saa moja usiku, paparazi wetu
alimfuata Diamond akiwa amesimama na Wema na kuwauliza kama kweli wana
nia ya kufunga ndoa.
“Hilo mwana mbona lipo wazi, nataka kumuoa staa na nataka kuzaa na staa,” alisema Diamond huku Wema akiwa hapingi.
MAMA WEMA ATANGAZA VITA NA DIAMOND Wakati
Dimaond akitambia ndoa na Wema, siku hiyohiyo ya Krismasi, mama wa Wema,
Mariam Sepetu alidaiwa kutangaza vita na mwanamuziki huyo baada ya
kusikia tetesi kuwa amerudiana na mwanaye.
Kwa mujibu wa rafiki wa
karibu wa mama Wema (jina tunalo) mama wa staa huyo alichukizwa na
kitendo cha Diamond kurudiana na mwanaye kwani anaamini anamchezea tu.
Mama wa Wema, Mariam Sepetu.
Rafiki huyo alizidi kudai kuwa, taarifa hizo zimemuweka mama huyo
kwenye wakati mgumu na kudai kuwa popote atakapokutana na mwanamziki
huyo atampopoa mawe au machungwa hata ikiwa siku ya ndoa yao.
“Mama
Wema amesema hampendi Diamond, popote atakapomuona itakuwa vita ya
wawili, kama kuna jiwe atamrushia, hata machungwa kama yapo yatakuwa
halali yake,” alisema rafiki huyo.
WOSIA WA MZEE SEPETU
Mpashaji huyo wetu alizidi kufunguka kuwa, mama Wema ana wosia mkononi
ambao aliuacha marehemu mumewe, mzee Isaac Abraham Sepetu.
Alisema
katika wosia huo, mzee huyo alisema hataki Diamond amuoe Wema na kama
mrembo huyo atakiuka wosia huo atapatwa na laana mbaya katika maisha
yake.
“Kinachomuumiza zaidi mama Wema ni huo wosia, mzee Sepetu
alisema hataki mtoto wake aolewe na Diamond, kama atakataa kuna kitu
kibaya kitamkuta katika maisha yake,” alisema rafiki huyo.
MAMA WEMA ASAKWA
Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili lilimvutia waya mama Wema ili
kuweza kuthibitisha madai hayo ambapo alisema kuwa, hayuko tayari
kuzungumzia jambo hilo kwa wakati huo mpaka atapoamua akisisitiza muda
si mrefu.
“Jamani nina mambo mengi sana ya kufanya na sijatulia
kabisa siko tayari kuzungumza chochote kwa sasa nikiwa tayari
nitawaambia kila kitu,” alisema mama Wema.