Google tag

mardi 14 février 2017

Diamond Platnumz athibitisha kuwa mbioni kumrudisha Q-Chief kwenye ramani

Diamond Platnumz amethibitisha kuwa amejipanga kumrudisha Q-Chief kwenye ramani ya muziki baada ya uongozi wake wa QS Mhonda kushindwa kufanya hivyo licha ya kudai kutumia zaidi ya shilingi milioni 200 bila kupata faida.
 Kwa muda kulikuwepo na tetesi kuwa Diamond ana mpango wa kumsainisha msanii huyo mkongwe kwenye label ya WCB. Na sasa, ingawa hajasema kuwa amepanga kumsanisha kwenye label hiyo, Diamond amekiri kuwa kwenye mipango ya kufanya kazi na legend huyo.
 

“Unajua lengo langu kama mimi au sisi vijana wa sasa hivi tunajaribu kuona tunavyoweza kufanya kazi kwa ushirikiano, so tuko na maongezi na bro tunaangalia tunawezaje kufanya kazi kwasababu ni mtu ambaye kwanza mimi namfeel halafu ambaye namuamini,” Diamond ameiambia Dizzim Online.

“Ni mtu ambaye najua kabisa yaani akibonyeza button hii basi huu mji mzima umechafuka. Kwahiyo siwezi kuyaongea mengi sema Watanzania watuombee dua tunachokiplan kifanyike vizuri,” ameongeza staa huyo.
Naye Q-Chief alisema, “mimi nahisi project inayofuata Simba anahusika kwasababu ni mtu ambaye ameniita kwa ushauri nikiwa na QS, amemuambia vitu vingi vya msingi, yeye shahidi hapa, lakini kama ni mtu anayeelewa mdogo wake ameniita amesema nini mpaka mimi nimeelewa na hajafanya maybe [QS] is not ready to do business but Diamond is a business man and I am ready to join a business man so long as kuna misingi. Lakini naamini ngoma inayofuata Diamond amenipa baraka zake.”

Hivi karibuni muimbaji huyo ambaye jina lake kamili ni Abubakar Katwila amekuwa kwenye vita vya maneno na kampuni inayomsimamia ya QS Mhonda anayoishutumu kwa kushindwa kumfikisha popote licha ya uwekezaji mkubwa ilioufanya kwake.

Ndugu zake pia walihoji kuhusu mkataba wa maisha aliosainishwa mtoto wao kwenye kampuni hiyo na kwamba tangu awe chini ya kampuni hiyo hawajaona mabadiliko ya maana kwenye maisha yake.

Nai (Model wa video ya Darassa): Mimi si msichana rahisi rahisi kwa wanaume

Rayvanny amtaja msanii wake mmoja wa TZ ambaye anatamani kufanya naye kolabo

Msanii wa muziki kutoka WCB, Rayvanny amedai msanii wa kundi la Weusi Joh Makini ndiye msanii ambaye anatamani kufanya naye kolabo.
 

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Rayvanny amedai bado hajazungumza na rapper huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Waya’.

“Bongo kuna wasanii wengi ambao ningependa kufanya nao kolabo lakini ukisema nimseme mmoja ambaye nawish ningefanya naye kitu ni Joh Makini,” alisema Rayvanny. “Joh namkubali sana na naona kama kuna kitu fulani chaajabu kitatokea nikifanya naye kolabo,”

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na kolabo ya wimbo ‘Kijuso’ aliyoshirikishwa na Queen Darleen, amedai bado hajafanya mazungumzo na Joh Makini kuhusu kolabo hiyo.
“Bado sijamwambia Joh Makini, lakini nadhani ukifika muda kila kitu kitafanyika. Kila kitu kitajulikana hapo lakini kama nikikutana naye nataka kufanya kitu tofauti sana,” alisema Rayvanny.

vendredi 3 février 2017

Michuano ya ligi kuu Uingereza wikendi hii

Chelsea wako kifua mbele katika ligi na alama 9 na wanaweza kujiimarisha kileleni wakati wakiipokea Arsenal ilio nafasi ya tatu.

Mechi hii kwa Chelsea ni fursa kujivua aibu baada ya kulambishwa sakafu na arsenal bao tatu kwa bila katika mechi ya awali.

Na baada ya hapo ndio ulikuwa mwanzo mzuri wa Chelsea kufululiza na matokeo mazuri .
Arsenal ambao jumanne walipokea kichapao cha Watford , wana wasiwasi mkubwa hasa baada ya kiungo wake Aron Ramsey kuumia mguu.

Pia watakosa huduma za Granit Xaka anayetumikia adhabu huku Mohamed Elneny akiwa michezo ya fainali za kombe la Afrika na timu yake ya Misr.

Ushindani pia ni kati ya washambuliaji wawili Diego Costa wa Chelsea na Alexis Sanchez ambao wanaongoza kama wafungaji bora na mabao 15.

Katika mechi nyingine hapo kesho Tottenham ilio nafasi ya pili wanaipokea Middlesbourg.

Nayo Liverpool itasaka ushindi wake wa kwanza mwaka huu wakiwa ni wageni wa Hull City .

Jumapili, Manchester City wanachuana na Swansea City huku Leicester City wakiikaribisha Man U

Nyumba ya Nicki Minaj yaporwa Marekani

Polisi kwenye jimbo la Los Angeles nchini Marekani wanachunguza wizi uliofanyika kwenye nyumba ya Nicki Minaj amabapo malia ya thamani ya dokl 175,000 iliibiwa.


Wizi huo ulitokea kwenye nyumba yake ya kifahari eneo la Beverly Hills lakini mwanamuziki huyo hakuwa nyumbani wakati huo.

Inaripotiwa kuwa nyumba hiyo ilivunjwa wakati wa uvamizi huo na baadhi ya nguo za Nicki Minaj kuibiwa.
Fanicha iliharibiwa huku picha na chupa za manukato zilivunjwa.
Bado haijulikani ni vipi waalifu waliingia nyumbani humo.

Waliiba vito vya thamani na bidhaa zingine zenye gharama ya dola 175,000.


Haya ndio maamuzi ya Frank Lampard kuhusu soka

Mchezaji wa zamani wa vilabu vya West Ham, Manchester City, Chelsea, New York City na timu ya taifa ya Uingereza Frank Lampard ambaye anamiaka 38, ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka na kusalia kuwa mtazamaji na kuchukua mafunzo ya Ukocha.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lampard ametoa uamuzi huo kwa kuandika ujumbe huu.

Frank Lampard ameshinda mataji matatu ya EPL, Makombe manne ya FA, vikombe viwili vya kombe la Ligi, Taji moja la Klabu Bingwa Ulaya na Europa, na kumfanya atimize michezo 1039 na Magoli 302 kwa miaka 21 aliyoitumikia kama mchezaji kwenye vilabu mbalimbali na timu yake ya taifa.