Google tag

dimanche 29 décembre 2019

Fred na Manchester United

FREDINHO.🔥⚽️

Huyu Mwamba hatajwi sana ndani ya Manchester United lakini kwa mtazamo wangu mimi binafsi ndio amekuwa mchezaji bora wa Manchester United katika kipindi cha takribani miezi miwili 



United ashinde au afungwe mara zote huwa anaonesha kiwango cha juu sana, energy level ya juu, passing , defending, interceptions ( anakata sana pasi zinazopita njiani kwenda kwao ) lakini pia anaanzisha mashambulizi haraka sana 

Anahitaji wachezaji wenzake wawe na ‘ consistency ‘ nzuri ili kazi yake izidi kutoa matunda na jana dhidi ya Burnley alikuwa Bingwa tena katikati ya kiwanja akisaidiana na Matic ambaye alionesha uzoefu wake.

Erling Haaland kwenda BVB

Taarifa zaidi .....

Straika wa kimataifa wa Norway Erling Braut Haaland ametua ndani ya klabu ya Borussia Dortmund kutoka RB Salzburg kwa dau linaloripotiwa kufika kiasi cha Pauni Milioni 18 na mkataba mpaka mwaka 2024. 



Haaland alikuwa akiwindwa na Juventus, Manchester United na RB Leipzig lakini ni Dortmund ndio wamefanikiwa kumnasa na atajiunga na wenzake Januari 3. 

Haaland mwenye umri wa miaka 19 msimu huu ameweka kambani magoli 28 katika mechi 22 pamoja na yale 8 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Future plan za CR7


Mreno mwenye myaka 33 na mchezaji nyota wa Juventus

Katangaza ya kwamba mchezo wa mpira wa miguu (Football) sio maisha yote
Bali kuna maisha mengine baada ya ku staff kucheza mpira wa miguu
Kasema : nataka kujiandaa kukisoma kingereza vizuri na kukielewa kiusawa, ili nikija Staff kucheza mpira niweze kuendeleya na mengine

Kasema : nataka niwe mchaza filamu

vendredi 27 décembre 2019

Kinda wa Inter Milan kusherekeya Goal

Jumamosi Disemba 21 mwaka huu katika mechi ya Serie A kati ya Inter dhidi ya Genoa Romelu Lukaku alimpa penati Sebastiano Esposito apige. Hilo likawa ni bao la kwanza kwa kinda huyo mwenye umri wa miaka 17 katika Serie A


Kilichotokea dogo akalia kwa uchungu sana na kwenda kushangilia kwa mama yake mzazi kutokana na furaha iliyopitiliza . . . 
Katika mechi hiyo waliyoibuka na ushindi wa mabao 4-0 Lukaku alifunga mabao 2 maana yake alijinyima Hat Trick akampa heshima bwana mdogo
.

Hilo likawa tukio kubwa la kihistoria kwa kinda huyo ambaye baada ya hapo alienda kujumuika na familia yake kusherekea kufunga mwaka kwa heshima ya kipekee. . . 

jeudi 26 décembre 2019

Vita ya Technique Kutoka kwa Samba Boys



Siku hizi katika soka tunaona jinsi gani msisitizo mkubwa ukizingatiwa kwa Magolikipa kuwa na uhitaji wa kuweza kutumia miguu yao vizuri kwenye kuanzisha mashambulizi ( Modern Goalkeeping )

Kuanzia kwa Victor Valdes ndani ya Barcelona ya Pep Guardiola mpaka Manuel Neuer akiwa Bayern Munich na timu ya Taifa ya Ujerumani na sasa ndio imekuwa utamaduni. 



Katika vikosi viwili Liverpool na Manchester City kuna Magolikipa wawili wa kimataifa wa Brazil ambao timu zao zinapata faida kubwa sana pindi wanapoanza mashambulizi kutoka nyuma , hata wakiwa wanashambuliwa wanageuka kuwa ‘ Sweepers ) hiyo inasaidia timu zao kuanza kukabia juu ya uwanja . 

Lakini swali kubwa baina ya Ederson Moraes na Alisson Becker ni Golikipa yupi yupo bora zaidi ya mwenzake wakiwa na mpira mguuni ?  ( wote wazuri lakini nani bora zaidi ya mwenzake ) 

A: Alisson Becker 
B: Ederson Moraes

Mzee aiba pesa na kuzitoa kama zawadi akisema 'Merry Christmas'

Bwana mmoja mwenye ndevu nyeupe alifanya uvamizi wa benki siku mbili kabla ya Krismasi na kuzirusha juu kwa furaha na kuwatakia kheri ya siku kuu wapita njia, mashuhuda wameeleza.
Polisi wamethibitisha "mwanaume mzee wa kizungu" alivamia benki ya Academy mjini Colorado Springs, Marekani siku ya Jumatatu.


"Aliiba pesa benki, akatoka nje na kuzitawanya kwa watu," shuhuda Dion Pascale alikiambia kituo cha Colorado 11 News.
"Alianza kurusha fedha kutoka kwenye begi na kisha akaanza kusema, 'Merry Christmas!'"
Kwa mujibu wa mashuhuda, mtuhumiwa huyo akapiga hatua chache kutoka benki na kuketi mbele ya mkahawa wa Starbucks akisubiri kukamatwa.
Katika hali ambayo inaweza kuwa ya kustaajabisha kwa wakazi wa Afrika Mashariki, wapita njia wanaripotiwa kuwa walichota fedha zote zilizozagaa na kuzirudisha benki.
Polisi wamemtaja mtuhumiwa huyo kwa jina la David Wayne Oliver, mwenye miaka 65 .
Polisi hawadhani kuwa alikuwa na usaidizi wowote.

mardi 24 décembre 2019

Hulk to Espagnole

Klabu ya Espanyol imeanza mchakato wa kumsaini mshambuliaji raia wa Brazil Givanildo Vieira de Sousa [ Hulk] kwa mkopo wa muda mfupi mpaka mwishoni mwa msimu huu. . .


Hulk ambaye kwa sasa anakipiga kunako klabu ya Shanghai SIPG ya China amefanikiwa kufunga mabao 10 na kutoa pasi za mabao 6 katika mechi 25 

Kenya : Un jeune étudiant crée le Bluetooth Chat fonctionnant sans internet pour concurrencer Whatsapp

Aujourd’hui, les services de messageries instantanées font partie intégrante de nos habitudes au quotidien. Sur le continent, les services de messageries tels WhatsApp ou encore Viber ont la cote. WhatsApp est sans doute le plus populaire de tous, sur le continent, le service de messagerie est utilisé pour discuter, partager des informations ou encore réaliser des affaires.

Smartphone (c) Droits Réservés

De nombreux africains ne peuvent plus se passer de WhatsApp. Le seul hic avec l’application, c’est qu’il faut acheter des données internet pour pouvoir l’utiliser. Un jeune étudiant kényan a trouvé la solution à cette problématique. Rogers Wambua est un jeune étudiant de l’Université des Sciences et Technologies de Masinde Muliro au Kenyan. Le jeune homme est un vrai mordu de tout ce qui touche à la technologie.

Wambua dans la ligne de mirre de Google

Comme de nombreux jeunes de son âge, Rogers utilise beaucoup les services de messageries instantanées dans sa vie au quotidien. C’est alors qu’il a eu l’idée de développer sa propre application de messagerie instantanée dénommée Bluetooth Chat. Ladite application est une merveille car elle peut fonctionner sans connexion internet. Grâce à Bluetooth Chat, Rogers a permis à ses camarades de l’Université d’échanger entre eux sans utiliser de connexion internet. «Mes camarades ont commencé par économiser leur argent de poche qu’ils utilisaient pour payer de la connexion pour s’écrire. Ils les consacrent à l’achat de livres et de nourritures» dira Rogers Wambua.

Le jeune inventeur a indiqué que son application peut être utilisée dans un rayon de 100 mètres. Rogers a pour ambition de renforcer les fonctionnalités de Bluetooth Chat en élargissant la distance de communication. Ainsi donc, les utilisateurs pourront communiquer avec leurs proches situés dans des zones reculées. Les entreprises de la Silicon Valley américaine ont déjà approché Rogers Wambua pour de futures collaborations.

Google et le Kényan collaborent déjà ensemble. Il faut noter que l’étudiant a pris le soin de breveter son application. «Je reçois actuellement un peu d’argent de Google annonces. Je vais mieux développer l’application et avoir davantage de gain» livrera le jeune homme qui pourra compter sur le soutien de personnes ressources pour renforcer les capacités du Bluetooth Chat avec pour but de l’intégrer dans le Google Playstore.

Totthenham yakata rufaa



Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amethibitisha ya kwamba 
klabu yake ya Totthenham imekata rufaa dhidi ya kadi nyekundu aliyoadhibiwa mshambuliaji wake Heung Min Son katika mechi ya kichapo cha 2-0 dhidi ya Chelsea siku ya Jumapili .

Hapo ni baada ya kumchzea rudiggee makosa na muamuzi kutowa kadi nyekundu baada ya kuchunguzwa kosa hilo na VAR

Mikel Arteta na mahitaji yake



Baada ya kutua ndani ya klabu ya Arsenal kocha Mikel Arteta amesema watafanyia kazi vitu vinne tu 


“ Mpira, Mchezaji mwenzako, Mpinzani na Nafasi “ 

(Ball, Teammate, Opponent and Space )

Mapenzi ya Neymar kwa dada yake

Mapenzi ya Neymar Jr kwa Dada yake ni makubwa mno na hayaelezeki lakini yamekuwa yanawatesa waajiri wake tena nyakati ambazo wanamuhitaji kuliko anavyofikiria.
.



Kila mwaka ifikapo mwezi machi tarehe 11 ni Siku ya kumbukumbu ya Siku ya kuzaliwa Dada wa Neymar aitwaye Rafaella santos😉.
.
Unajua anachokifanya Neymar ikifikaa miezi hii na tarehe karibia na Siku ya kuzaliwa Rafaella.
.
Kwa lugha nyepesi za watoto wa kiswahili wanaita 'Kujivunja' yaani anajiumiza kwa makusudi ,kama sio kufanya hivyo basi atafanya kosa lolote ili tu apewe adhabu itakayomfanya akosekane eneo la kazi tarehe ya Siku ya kuzaliwa Rafaella.
.
Amefanya Mara kadhaa akiwa Barcelona hata Paris Saint Germain pia,.
.
Baadhi ya Siku ambazo amekosekana ili akahudhurie Siku ya kuzaliwa Dada😃.
.
Akiwa Barca.
1⃣11 machi 2015-alisimamishwa.
2⃣11 machi 2016-alisimamishwa.
3⃣11 machi 2017-aliumia.
.
Akiwa Paris
1⃣11 machi 2018-aliumia.
2⃣11 machi 2019-aliumia.
.
Nawakumbusha tu 11 machi 2020 ni Dortmund na PSG mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya😃 yetu macho tu!.

lundi 23 décembre 2019

Cavani Kutua Atletico:



Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay Edinson Cavani amekubali mkataba wa miaka mitatu kujiunga na Atletico Madrid mwezi Januari 2020


Cavani mkataba wake na PSG unafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu. 

Tuzo barani Afrika


Wana fainali watatu walioteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka barani Afrika 

1: Mo Salah 
2: Riyad Mahrez
3: Sadio Mane 



Mshindi atatangazwa siku ya Jumanne , Tarehe 07 Januari 2020 , Hurghada, Egypt.

Flick kuendelea kuinoa Bayern.


Klabu ya Bayern Munchen imethibitisha, kocha wa muda Hansi Flick ataendelea kuinoa klabu hiyo hadi mwishoni mwa msimu huu wa 2019/20.


Rekodi ya Thierry Henry , EPL

Gwiji wa klabu ya Arsenal Thierry Henry ndio mwanaume pekee aliyefanikiwa kuwa na assists 20 katika msimuy mmoja wa Ligi alifanya hivyo msimu wa 2002/03 mpaka sasa hakuna kiumbe aliyewahi kufikia.

Je msimu huu inaweza kuvunjwa ?? Kiungo mshambuliaji wa Man City Kevin De Bruyne jana baada ya kutengeneza goli amefikisha assists 10 msimu huu mpaka zikiwa zimepigwa mechi 17 , zimebaki mechi 21 . Ataweza kutengeneza magoli 10 mengine katika mechi 21 zilizobaki ??